Pichani
kati ni Mratibu wa shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,Antu
Mandoza akiwataja vinara watatu kati ya 14 walioshindana vikali ndani ya
ukumbi wa Sunciro usiku wa kumkia leo.Kutoka shoto ni Joh Maker
(Morogoro),Ney Lee (Mbeya), sambamba na kijana mdogo lakini ni mwenye
kipaji cha kufoka ile mbaya kutoka jijini Mwanza aitwaye Young
Killa.Shindano hilo lilikusanya vijana mbalimbali wenye kipaji cha
kuimba kutoka mikoa kadhaa ikiwemo Mbeya,Arusha,Morogoro,Tanga,Dar Es
salaam,pamoja na jiji la Mwanza. Washiriki hao watatu watapa nafasi ya
kuendelea kuonesha vipaji vyao kwenye matamasha yote ya Serengeti Fiesta
2012,ambayo inatarajia kuanza kurindiama Ijumaa ya wikii hii ndani ya
jiji la Moshi-Chuo cha ushirika na jumipili litafanyika Uwanja wa
Mkwakwani mkoani Tanga
Burudani
iliokuwa ikiendelea kutolewa na dani ya ukumbi wa Sunciro,washabiki
walikuwa wakijimwa mwaya kwa staili hiyo huku wakiendelea kushuhudia
shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota,lililokuwa na ushindani mkubwa
kwa washiriki.
Mshiriki
wa shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,Catrina kutoka jijini
Arusha akionesha kipaji chake cha kuimba mbele ya umati mkubwa (haupo
pichani) uliokuwepo kulishuhudia live tukio hilo ambalo pia lilikuwa
likirushwa live na Clouds TV na Redio.
Majaji
wa shindano hilo wakijadiliana jambo,kutoka kulia ni Othman
Suka,Prodyuza wa Muziki Dunga,Dj Ibra pamoja na mtaalamu wa mambo ya
muziki kituo cha THT,Kardinal Gentlo.
Baada
ya kuchuana vikali,washiriki 14,ukapitishwa mchujo mkali na kuwapata
hawa washiriki sita pichani kama waonekanayo.Kutoka kulia ni Candy
(DSM),Bridan Khan (Tanga),Ney Lee (Mbeya),Joh Maker (Morogoro) pamoja na
You Killa kutoka Mwanza.
Ilikuwa ni full kushangweka ndani ya ukumbi wa Sunciro.
Mshiriki
wa shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,Joh Maker kutoka mkoani
Morogoro akionesha umahiri wa kipaji chake cha kufloo mbele ya sehemu
ya mashabiki waliofika kulishuhudia live tukio hilo ambalo pia lilikuwa
likirushwa moja kwa moja na Clouds TV na Redio.
Mshiriki
wa shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,Candy kutoka jijini Dar
akiimba na kucheza kwa umahiri mkubwa mbele ya sehemu ya mashabiki
(hawapo pichani) waliofika kulishuhudia live tukio hilo ambalo pia
lilikuwa likirushwa moja kwa moja na Clouds TV na Redio.
Mshiriki
wa shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,Ney Lee kutoka mkoani
Mbeya akiimba na kucheza kwa umahri mkubwa mbele ya sehemu ya mashabiki
(hawapo pichani) waliofika kulishuhudia live tukio hilo ambalo pia
lilikuwa likirushwa moja kwa moja na Clouds TV na Redio.
Mmoja
wa majaji,Dj Ibra akifafanua jambo kwa washiriki wa shindano
la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,shoto kwake ni mtayarishaji wa
muziki aitwaye Dunga.
Mchakato
wa majaji ulikuwa mgumu kuwapata vinara husika wa shindano hilo,kwani
kila mmoja alijitahidi kuonesha uwezo na kipaji alichonacho.Kwa mujibu
wa majaji wa shindano hilo walitoa vigezo husika kwa washiriki kuwa ni
umiliki wa jukwaa na kujiamini,ubunifu wake wa kuimba,kuwepo mawasiliano
kati yake na mashabi wanaotazama na pia kutoa maneno fasaha ili
yasikike.
Washabiki
mbalimbali walijitokeza kwa wingi kushuhudia shindano la Serengeti
Fiesta Supa Nyota 2012,lililofanyika ndani ya ukumbi wa Sunciro jijini
Dar,shindano hilo limefanyika likiwa na lengo ya kuinua vipaji vya
kuimba kwa vijana kutoka sehemu mbalimbali,ambapo pia ilikuwa ni sehemu
mojawapo ya mchakato wa kuanza kwa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
No comments:
Post a Comment