skip to main |
skip to sidebar
JOSE MOURINHO AENDELEA KUVUNJA REKODI DUNIANI - AWA KOCHA WA KWANZA KUCHUKUA MAKOMBE YA LIGI NA SUPERCUP KWENYE NCHI NNE ZA JUU KISOKA
Kocha
Jose Mourinho ameendelea kuvunja rekodi mbalimbali katika ulimwengu wa
soka, baada ya kuwa ndio kocha pekee aliyechukuwa ubingwa ligi kuu za
nchi nne tofauti kubwa barani ulaya na vilabu vya Porto, Chelsea, Inter
Milan na Real Madrid.
Usiku wa kumakia leo Jose Mourinho
alikiongoza kikosi chake cha Real Madrid kuwafunga mahasimu wao wakubwa
FC Barcelona bao 2-1 kwenye mchezo wa pili wa kogembea kombe la Supercup
kwenye uwanja wa Santiago Bernebeu. Kwa matokeo hayo timu hizo
zikafunga kwa jumla ya mabao 4-4, lakini kutoka na Madrid kuwa na idadi
kubwa ya magoli ya ugenini wakatwaa ubingwa huo wa tatu tangu Mourinho
afike Bernebeu.
Kwa maana hiyo baada ya kufanikiwa
kutwaa uchampion huo wa Supercup, Mourinho anaweka historia nyingine
kubwa duniani akiwa ndio kocha pekee kuwahi kutwaa makombe ya ligi na
supercup - (ambalo hukutanisha bingwa wa ligi na bingwa wa kombe la FA
ya nchi husika -au mshindi wa pili wa ligi) katika nchi nne tofauti
zilizo juu kwenye viwango vya FIFA - England alichukua EPL na Community
shield, Ureno walifanya hivyo hivyo, Italia pia na sasa Spain.
No comments:
Post a Comment