Katibu
wa Chama cha Damokrasia na Maendeleo Mkoani Morogoro, Abel Luanda
ametoa tamko rasmi la kujiuzu nafasi hiyo na kuahidi kutoa taarifa ya
chama atakachohamia mapema wiki ijayo.
Luanda
alitoa tamko hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini
hapa na kutaja sababu tano zilizomsababisha kuchukua maamuzi hayo
aliyoyaita kuwa ni magumu katika siasa.
Alizitaja
sababu hizo kuwa ni kupisha upepo mbaya wa kisiasa ndani ya Chadema
kuanzia ngazi ya mkoa hadi taifa, kukosa ushirikiano na mwenyekiti wa
Chadema mkoa Susan Kiwanga ambaye ni mbunge wa viti maalumu wa chama
hicho mkoani hapa pamoja na dharau iliyojengwa na viongozi wakuu wa
chama hicho kitaifa dhidi ya viongozi wa mkoa.
Sababu
nyingine alieleza kuwa ni kupisha agenda ya siri iliyofichika ndani ya
M4C inayolenga kuwaondoa viongozi fulani ndani ya mkoa na wilaya
wanaoonekana kuwa na misimamo ya kupinga kambi fulani inayojiandaa na
uchaguzi mkuu wa chama hapo mwakani.
Vilevile
alisema kuwa sababu iliyomfanya ajiuzulu ni pamoja na viongozi wa ngazi
ya chini kuanzia kata, jimbo, wilaya hadi mkoa kutumiwa kama muhuri
huku wakitakiwa watimize wajibu mkubwa wakati mtetezi wa haki zao
hayupo.
“Mimi
naondoka lakini nawaachia ujumbe mmoja kuwa Chadema siyo yenu ninyi
viongozi wachache ambao mpo hapa kwa dhamana tu nanyi mtapita kama
waasisi wa chama hichi waliopita, lakini nawaachia chama kikiwa salama
na imara” alisema Luanda.
Aidha
alisema kuwa yeye si mgeni kwenye siasa kwani aliwahi kuwa mwanachama
wa NCCR- Mageuzi na baadaye alihamia Chadema na kupata nafasi ya udiwani
mwaka 2005-2010 wa kata ya Kibungo juu ambapo alisema kuwa katika
nafasi hiyo aliweza kukiimarisha Chadema kuanzia ngazi ya tawi hadi
mkoa.
Alisema
kuwa kutokana na mema aliyoyafanya kwa Chadema anaamini kuwa wapo
viongozi wengine wa chadema wa ngazi mbalimbali watakaounga mkono
maamuzi yake na kuachia ngazi hivyo aliwataka kutoogopa kukihama chadema
kwani wanaweza kufanya siasa kwenye chama chochote.
Alipotakiwa
kueleza kama anania ya kuhamia CCM Luanda alisema kuwa kwa sasa
anaangalia upepo wa kisiasa na muda si mrefu atatangaza ramsi chama
atakachohamia huku akisisitiza kuwa atahamia chama ambacho kitakuwa na
misimamo na chenye kufuata katiba na miongozo na sio kupigana majungu na
fitina.
No comments:
Post a Comment