Mkuu wa
wilaya ya Rungwe Mh. Crispin Meela akizungumza na Mashabiki, Wadau na
Wananchi wa Rungwe wakati wa uzinduzi wa Kongamano la kuifufua timu ya
Tukuyu Star kwenye uwanja wa Tandale mjini Tukuyu mkoani Mbeya leo,
ambapo kulikuwa na michezo mbalimbali ya mpira wa miguu ikishereheswa na
ngoma za asili ya watu wa Rungwe ya Ighoma iliyokuwa ikutumbuizwa
katika viwanja hivyo, Bonanza lilivuta hisia za watu wengi na wadau wa
mkoa wa mbeya na mikoa ya jirani hasa wachezaji waliowahi kuchezea timu
ya Tukuyu Star miaka ya 1980 na 1986 huku umati wa watu ukishuhudia
tukio hilo. Katika bonanza hilo timu ya Rungwe Veterani imefaikiwa
kkuichapa timu ya wadau wa Tukuyu Star Family magolo 3-1, akielezea
mpambano huo Kocha wa timu ya Tukuyu Star Family Kenny6 Mwaisabula
amesema kushindwa ni sehemu ya mchezo, lakini pia wachezaji wa Rungwe
Veterani wako fiti zaidi kimchezo kutokana na kwamba muda mwingi
wanafanya mazoezi sana, lakini pia hali ya hewa inawaruhusu kwani
wamezoea baridi tofauti na wachezaji wake, Usiku huu kuna kongamano
linaendelea mjini Tukuyu ili kujadili mikakati mbalimbali na utaratibu
utakaotumika katika kuiendesha Tukuyu Star mpya. |
|
|
No comments:
Post a Comment