Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, August 24, 2012

Mapenzi siyo presha, ila presha inaletwa na mpenzi uliyenaye



Nakubaliana na wewe kwamba mapenzi yamekuwa magumu. Nakuunga mkono kwa asilimia 100 kuwa wakati mwingine yamekuwa ni mzigo mzito kuubeba. Hata sikubaliani na wewe ukisema mapenzi ni presha.
Nakiri kuwa mapenzi yanaendelea kujeruhi wengi, bado ni mateso kwa wengine. Sasa hivi, asilimia kubwa ya watu, inaamini kwamba kupata mwenzi sahihi wa maisha ni ndoto za alinacha. Ni kamari, ni bahati nasibu. Sipingi.
Maendeleo yamekuja na mambo leo. Kile kinachoonekana ni uzungu, kimeathiri kwa kiasi kikubwa ustaarabu wetu. Mila na desturi zetu, vimepokwa na utandawazi uliotujia. Hii inamaanisha kwamba uhusiano wa kimapenzi wa sasa, hauendani na sura ya utamaduni wetu.
Vijijini kuna unafuu japo na kwenyewe fujo zimeshaingia na mambo yameshabadilika. Mijini ndiyo matatizo yenyewe. Ulimwengu wa digitali na fursa za mitandao zinatutia wazimu. Tunataka kuiga mitindo ya maisha ya wenzetu, matokeo yake tunageuka watumwa wa mapenzi.
Hayakuletwa mapenzi ili yawaumize watu, yapo kwa ajili ya kutoa faraja ndani ya jamii. Yalivyo ni kwamba baada ya misukosuko ya kimaisha, vurugu mechi za kusaka riziki na mihangaiko mingine ya kimaisha, angalau unaweza kusahau yote unaporejea kwa mwenzi wako.
Hata hivyo, mapenzi hugeuka matatizo pale ambapo kazini umeondoka pakiwa moto, unarudi nyumbani nako pia unakuta moto. Unakosa sehemu ya kwenda kujishikiza. Faraja inaota mbawa. Hapa ndipo tafsiri ya mapenzi inapokosa mashiko. Jitazame, muangalie na mwenzako!
Japo ni ukweli usiopingika kuwa mapenzi siku zote hayapo tambarare hata kwa wenza waliostaarabika, ila katika kundi la mabrazameni na masistaduu ni mtihani. Kuna usemi kwamba glasi hugongana kabatini, nakubaliana nao lakini kwa makundi hayo ni pasua kichwa.
Presha inaletwa na aina ya wapenzi. Mabrazameni na masistaduu ni zao la mapenzi ya Kichina, yaani uhusiano bandia. Inawezekana akiwa kwako akajilegeza kama amefika, kumbe anao wengine wengi. Hili ni janga zito kwa maisha ya sasa. Uaminifu haupo, uzinzi na usaliti vimekuwa fasheni ya kutukuzwa.
Wengine siyo masistaduu wala mabrazameni, wapo kawaida au pengine wana muonekano wa heshima mno. Hata hivyo, ukichimbua hulka zao ndiyo utachoka. Ni wakali wa kuwapanga foleni, akitoka kwa huyu anakwenda kwa yule. Mapenzi yametawaliwa na rangi ya Shetani.
Wapo wanaobadili wapenzi kwa sababu za tamaa, lipo kundi linaloamini miili yao ni mtaji wa kupata fedha, wengine shida za maisha, zikasababisha uamuzi huo wa kujidhalilisha, wapo ambao ni tabia. Bila kugusa huku na huko hatosheki. Makundi yote hayo yamezingirwa na Ibilisi.
Mume wa mtu, anapewa sifa ya ‘uchapaji’ wa vidosho. Kwamba anajua kuwapanga kila kona. Nyumba za kulala wageni, anaingia kama nyumbani kwake. Yaani wanamjua, ni mteja wao hodari. Akifika, wanampeleka kwenye chumba anachokipenda.

Wapo wanaopiga simu, yaani namba za nyumba za kulala wageni zimejaa kwenye simu yake. Akijibiwa kwamba Sinza Kumekucha hakuna vyumba, anapiga Vatican, nako akikosa anajaribu Mori. Inahitaji sala na dua kuishi na mtu wa aina hiyo. Kuna mawili, kama hatakupa maradhi, omba usijue tabia yake, atakuua kwa presha.
Mke wa mtu mkali wa mafiga matatu mpaka matano. Anaita vidumu. Anaingia hoteli na gesti bila woga. Wapo wanaodiriki kuwaingiza wanaume ndani ya nyumba zao, wakati waume zao wakiwa hawapo. Balaa likamkuta yule mwanamke wa Kenya, akagandiana na mwanaume aliyemuingiza chumbani kwake, juu ya kitanda anacholala na mumewe.
Wengine ni ujasiri wa asili, wapo wanaofanya hivyo kwa sababu wanaona fasheni. Katika kundi hili wanaorukaruka, wakijiona ni fasheni ndiyo shabaha yangu kubwa. Itapendeza zaidi mapenzi yakikaa kwenye mstari wake ulionyooka. Maana halisi isipindishwe.

Kama ambavyo Jennifer Lopez, anavyobadili wanaume Marekani, eti na hapa Bongo, Wema Sepetu naye hajambo. Nimeshazungumza mara nyingi na Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006-07, hata siku moja hajawahi kuonesha kujuta kwa safari yake ya kubadili wanaume ovyo.
Naseeb Abdul ‘Diamond’, Jumanne Kihangala ‘Mr. Chuz’ na wengine mfano wao, kama Sean Combs ‘P. Diddy’, Christiano Ronaldo na wengineo. 
Stori na: GPL

No comments:

Post a Comment