Na Gladness Mallya
KUTOKANA
na kuzidi kwa wimbi la mastaa wa Kibongo kuugua na kulazwa mwaka 2012
katika hospitali mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi, daktari
aliyeomba hifadhi ya jina lake ameeleza sababu na kusema wapo hatarini
kuzeeka mapema, Amani lina ripoti kamili.
Gazeti
hili lilizungumza na daktari huyo anayefanya kazi katika hospitali moja
kubwa hapa nchini ambapo alisema sababu zinazowafanya mastaa wengi
kukumbwa na magonjwa mbalimbali ni uzee, vyakula wanavyokula, kutofanya
mazoezi na kutokuwa na mazoea ya kupima afya zao mara kwa mara.
“Unajua
mastaa hawa wakishapata umaarufu, basi wanabweteka. Hawafanyi mazoezi,
wanapenda vyakula vyenye mafuta mengi wakidhani wanakula
vizuri kumbe wanajiharibu,” alisema dokta huyo.
Mastaa
wengi waliolazwa kwa mwaka 2012 walikuwa wakisumbuliwa zaidi na
magonjwa kama presha, tumbo, kifua, malaria na mengine mengi ambapo hapa
tunakuletea listi ya mastaa hao na magonjwa yaliyokuwa yanawasumbua.
WEMA SEPETU
Hivi
karibuni Wema alilazwa katika Hospitali ya Heamed iliyopo Upanga, Dar
akisumbuliwa na tatizo la kubanwa kifua ambapo hali yake ilikuwa mbaya
kiasi cha kuwafanya Watanzania wamuombee.
NASIBU ABDUL ‘DIAMOND’
Diamond
aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake Sinza-Mori, Dar ambapo alikimbizwa
kwenye Hospitali ya Heamed na kulazwa akisumbuliwa na homa kali na
uchovu uliosababishwa na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika.
SAID NGAMBA ‘MZEE SMALL’
Mkongwe
huyo wa maigizo na filamu anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza ambapo
alilazwa Muhimbili, Dar na baadaye aliruhusiwa lakini hadi sasa bado ni
mgonjwa.
COLETHA RAYMOND ‘KOLETA’
Hivi
karibuni mwigizaji huyo alilazwa kwenye Hospitali ya Kairuki iliyopo
Mikocheni, Dar akisumbuliwa na ugonjwa wa kidole tumbo ‘appendix’ ambapo
alifanyiwa upasuaji na kupoteza fahamu kwa takribani saa saba.
TAMRINA POSHI ‘AMANDA’
Wiki mbili zilizopita Amanda alilazwa katika Hospitali ya Aga Khan, Dodoma kutokana na kusumbuliwa na presha kushuka.
RUTH SUKA ‘MAINDA’
Mwigizaji
Mainda alilazwa kutokana na kusumbuliwa na presha ya kushuka ambapo
alidondoka ‘lokesheni’, tatizo hilo likaendelea kumsumbua mara kwa mara.
JUMA KILOWOKO ‘SAJUKI’
Mwigizaji
Sajuki alilazwa nchini India akisumbuliwa na uvimbe tumboni ambapo
baada ya matibabu alirejea Bongo na mpaka sasa bado hajawa fiti vya
kutosha.
WASTARA JUMA
Mwigizaji
Wastara ambaye ni mke wa ndoa wa Sajuki naye alilazwa nchini India
wakati alipokwenda na mumewe kwa ajili ya kumhudumia.
HUSNA IDD ‘SAJENTI’
Wiki iliyopita mwigizaji huyo alilazwa huko kwao, Kondoa-Irangi, Dodoma akisumbuliwa na homa ya mapafu.
kwa Hisani Global publisher
No comments:
Post a Comment