Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 9, 2012

BALOZI MAHALU ASHINDA KESI YAKE YA UHUJUMU UCHUMI ILIYOKUA INAMKABILI

Taarifa zilizotufikia punde kutoka mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam,  Balozi Mahalu ameshinda keshi iliyokuwa ikimkabili ya ununuzi wa nyumba ya ubalozi wa Tanzania nchini Italia,ameshinda kesi hiyo hana hatia  tarifa zaidi na picha  fuatilia Fullshangweblog.
Waandishi wa habari wakimfuata Balozi Profesa Mahalu akiwa pamoja na Mdogo wake Mirasi Rama wakitoka nje ya Mahakama ya Kisutu Mchana huu mara baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili akidaiwa kununua nyumba ya Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Akisoma hukumu iliyosomwa  kuanzia Saa sita leo na  Hakimu Mfawidhi mkazi wa mahakama ya Kisutu Mh. Ilivin Mugeta imemtoa Balozi Profesa Mahalu katika hatia na kumwachia  huru (PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWEBLOG)
Balozi Profesa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushinda kesi yake katika mahakama ya kisutu leo.
Wakili wa Balozi Profesa Mahalu Bw. Alex Mgongolwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mteja wake kushinda kesili iliyokuwa ikimkabili kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Balozi Profesa Mahalu katikati akitoka nje ya mahaka ya Kisutu huku akiwa ameongozana na mdogo wake Mirasi Rama kulia ni Wakili wa kujitegemea Mabere Nyaucho Marando.

Picha na Full Shangwe Blog

No comments:

Post a Comment