Erick Evarist na Gladness Mallya
HUJAFA, hujaumbika! Hali ya staa wa vichekesho na filamu Bongo, Said Mohamed Ngamba ‘Mzee Small’ bado hairidhishi tangu mwezi Mei, mwaka huu alipopatwa na ugonjwa wa kupooza ghafla nyumbani kwake Tabata-Kimanga jijini Dar es Salaam, Ijumaa Wikienda linafunguka.
Mzee Small alipatwa na ugonjwa huo wakati akitokea mkoani Mwanza alipokwenda kufanya kampeni ya kupinga mauaji ya albino, safari ambayo aliambatana na mkongwe mwenzie kwenye sanaa, Bi Chau.
TUJIUNGE NA MKEWE
Akizungumza na Ijumaa Wikienda lilipofika nyumbani kwake kumjulia hali, mke wa staa huyo, Fatuma Said alisema siku mumewe alipopata matatizo alifika salama na kuanza shughuli zake za kila siku lakini kesho yake, ghafla alishtuka kumuona mumewe ametokewa na hali hiyo (kupooza) ghafla.
Alisema kuwa mara baada ya kufikishwa kwenye Hospitali ya Amana, Dar, madaktari walimcheki na kugundua alipatwa na stroke (kupooza) ndipo matibabu yakaanza.
BADO HALI TETE
Akizungumzia afya yake, Mzee Small alisema: “Kwa kweli nilitakiwa kurudi hospitali kwa ajili ya kuchekiwa upya na kufanyiwa mazoezi tangu Julai 5, mwaka huu lakini kwa kuwa sikuwa na fedha sikuweza kwenda hivyo bado hali ni mbaya na naomba Watanzania wanisaidie.”
KUTOKA KWA MHARIRI
Kwa kutambua kuwa Mzee Small kwa sasa anashindwa kuendelea na kazi zake kutokana na ugonjwa huo, ni wazi kuwa anahitaji msaada wa kuweza kujikimu kwa matibabu.
Kama unagushwa kumsaidia Mzee Small, basi tuma chochote ulichonacho kwa njia ya M-Pesa kwa namba yake ambayo ni 0754 647265.
SOURCE GLOBAL PUBLISHER
No comments:
Post a Comment