Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, August 21, 2012

NYUMBA ZACHOMWA MOTO NA KUVUNJWA WILAYANI MAGU KWA MADAI YA KUVAMIA HIFADHI YA SAKAYA



Katibu Mkuu wa ADC Lukas Limbu akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani  kuhusiana na tukio la wananchi wa vijiji Bugatu, Misungwi na Mwabulunga kuvunjiwa nyumba  na kuchomwa moto kwa madai ya kuvamia na kuishi ndani ya Hifadhi ya taifa ya Sakaya wilayani Magu Agosti 2, mwaka huu.
Philipo James akiwa amekaa kandokando ya  mabaki ya nyumba zake mbili zilizoteketezwa kwa moto na  anadai wake zake wawili wamemkimbia na kumwacha na watoto wake wanne
Moja ya famili ya mzee Manhe Mayoka ikiwa imejifadhi katika kibanda kibovu ambacho hakijaezekwa baada ya nyumba zao nne kuvunjwa na kuchomwa moto katika kijiji cha Bugatu Magu wakidaiwa kuvamia na kuishi ndani ya hifadhi ya taifa Sayaka kinyume cha sheria.
Mama akiwa hana  la kufanya akiwa katika kibanda abacho kimekuwa makazi yao kufuatia nyumba yao kuvunjwa na kuchomwa moto ,hapa akiwa na watoto wake wawili.
Kijana akiingia katika banda ambalo wanalitumia kulala baada ya nyumba zao kuvunjwa huko Mwabulenga Magu juzi
Katibu wa ADC akiangalia moja ya makaburi yaliyokutwa eneo linalodaiwa kuwa hifadhi ya taifa Sakaya.Kaburi hilo ni la mwaka 1966 ambalo ni la moja ya familia iliyovunjiwa nyumba 9 kwa madai ya kuvamia hifadhi hiyo
Katibu wa ADC , Lukas Kadawi  (mwenye suti nyeusi ) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya familia ya Ester Kihuruma (kushoto kwa katibu huyo wa ADC ) , alipokwenda kuwapa pole wahanga wa tukio la kuvunjiwa nyumba zao wakidaiwa kuvamia hifadhi ya Sakaya.
Mkuu wa Wilaya ya magu, Jaqueline Liana akisistiza jambo kuhusiana na tukio la kuvunja nyumba za wakazi wa vijiji vya Bugatu, Mwabulunga, salama, Kitongo, Misungwi na Lugata wakidaiwa kuingia ndani ya hifadhi kinyume cha sheria

No comments:

Post a Comment