Samuel Eto'o amekataa kuichezea
Cameroon katika kutekeleza mgomo wake dhidi ya kile alichokiita
"mpangilio mbovu na mazingira yasioeleweka" katika kikosi cha timu ya
taifa.
Mshambuliaji huyo alikuwa kwenye kikosi cha Cameroon kwa
ajili ya kupambana na Carpe Verde katika michuano ya kufuzu kombe la
mataifa ya Afrika mwezi September baada ya kumaliza adhabu yake
kufungiwa miezi nane.
Lakini Eto'o alisema kwenye barua yake
aliyoiandikia shirikisho la soka la Cameroon hatoweza kurejea kwenye
timu ya taifa kwa sababu matatizo yote yaliyomfanya akafungiwa bado
hajatafutiwa ufumbuzi.
Eto'o, ambaye ameshaichezea nchi yake
mechi 109 na kufunga mabao 54, alifungiwa kutokana na kuongoza mgomo wa
wachezaji baada ya kutolipwa posho zao.
Shirikisho la soka la
Cameroon liliamuarifu Eto'o na mwanasheria wake pamoja na timu yake ya
Anzhi Makhachkala kwamba kifungo chake kimeisha mapema wiki hii.
Na
kocha Denis Lavagne akamchagua Eto'o katika kikosi chake cha wachezaji
23 kwa ajili ya kucheza dhidi ya Cape Verde tarehe 8 mwezi ujao kwenye
mchezo wa raundi ya kwanza ya kufuzu kushiriki AFCON 2013.
Lakini
nahodha wa Cameroon bado amekosa furaha dhidi ya masuala ya uongozi
mbovu kwenye timu ya taifa na suala lao la kuwapandisha wachezaji ndege
daraja la pili tena kwenye safari ndefu - na kutokana na sababu hizo
mshambuliaji huyo wa zamani wa Barca amejiondoa kwenye timu ya taifa.
"Timu
yetu ya taifa inaendelea kupotea kutokana na mazingira mabovu na
mpangilio usioleweka kwenye timu ya taifa - vitu ambavyo haviendi sawa
na michezo ya kisasa," aliandika Eto'o katika barua yake kwenye kwa CFF
ambayo pia imewekwa kwenye mtando wake.
"Nina mashaka washabiki
wa timu ya taifa wataelewa hatua yangu hii ambayo mlengo wake mkuu ni
kubadilisha mambo yote ya hovyo kwenye timu ya taifa na kuyafanya kuwa
bora.
"Timu ni taasisi yenye heshima ambayo imechangia sana mafanikio ya nchi" - alimaliza Etoo.
WAZIRI BITEKO KUFUNGUA MKUTANO MKUU WA SABA WA JUMUIYA MAMLAKA ZA USIMAMIZI
WA USAFIRI MAJI AFRIKA
-
Na Lilian Ekonga. Dar es salaam.
Tanzania kupitia shirika la uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeteuliwa
kuwa nchi mwenyeji kwenye wa Makutano wa ...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment