WANANCHI
waishio mpakani mwa Tanzania na Uganda wameingia na hofu baada ya
kugundulika kuwa ugonjwa hatari wa Ebola imeingia nchini.
Watu
wengi mkoani hapa kuanzia juzi walionekana kuingiwa na wasiwasi baada
ya taarifa kuzagaa kuwa mgonjwa mmoja amelazwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Karagwe ya Nyakahanga, mkoani hapa.
Wengi walisikika wakishauri serikali za Uganda na Tanzania kushirikiana kudhibiti ugonjwa huo usizidi kusambaa zaidi.
Inaelezwa
kuwa mgonjwa huyo aliingia nchini akitokea nchi ya Uganda na kwamba
hivi sasa amelazwa katika Hospitali ya hiyo chini ya uangalizi maalumu
wa madaktari.
Wananchi wazungumza
Wananchi
hao walisema kuwa katika maeneo kama Mutukula ni vigumu sana kudhibiti
mtu mwenye ugonjwa asiwaambukize wengine kutokana na mwingiliano mkubwa
wa kibiashara uliopo.
Mkulima
katika eneo hilo lililopo Wilaya ya Missenyi, Samihu Majidu alisema
kuwa tangu walipotangaziwa kuchukua tahadhari, wanaishi kwa wasiwasi,
wanaogopa kugusana na kushikana mikono.Naye, Sauda Hassan, Mtanzania
anayefanya biashara katika eneo la Mutukula alisema
kuwa hata kama watakuwa makini kivipi, lakini bado vyombo vya usafiri ni tatizo kubwa linaloweza kueneza ugonjwa huo kwa kasi.
“Wenyewe mnaona hali ilivyo, watu wa Mbalala, Busia (Uganda) wako hapa, kama mtu ana ugonjwa utazuiwa vipi?” alihoji.
Aliongeza:
“Wanakuja wamebanana kwenye magari wakati tunaambiwa msigusane, magari
yanajaza sana abiria wengine wanasimama.”Sauda alisema: “Tunafanya
biashara hapa, mteja anakuja anakupa hela unashika bila kinga yoyote
kama mteja ana ugonjwa ukashika hela ambayo ina majimaji utaugua,
Nadhani tununue mipira ya kuvaa mikononi wakati wa kufanya biashara
maana tukisema tuache biashara uchumi utashuka.”
Alisema hata kama Serikali itafunga mpaka wa nchi hizo bado tatizo litakuwepo kutokana kuwepo kwa njia nyingi za panya.
Akizungumza
na Mwananchi Jumapili jana, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Nyakahanga, Dk Andrew Cesari alikiri kupokea mgonjwa mwenye dalili
zinazowiana na za ugonjwa wa ebola.
Alisema mgonjwahuyo alipelekwa hospitalini hapo akitoka eneo la Kyerwa ambalo lipo mpakani na nchi hiyo ya Uganda.
Alisema mgonjwahuyo alipelekwa hospitalini hapo akitoka eneo la Kyerwa ambalo lipo mpakani na nchi hiyo ya Uganda.
Dk Cesari alisema kuwa mgonjwa huyo alikuwa ana homa kali, alivuja damu sehemu mbalimbali za mwili wake na kutaapika.
Daktari
huyo alisema kwa mujibu wa maelezo ya ndugu zake, mgonjwa huyo alianza
kupatiwa matibabu nyumbani kwao na alipoonekana kuzidiwa ikibidi
wampeleke hospitalini hapo.
Alisema mgonjwa huyo alipokelewa katika chumba maalum na kupelekwa katika wodi ya magonjwa hatari ambapo ametengwa na anaendelea vizuri. “Damu sasa imesimama kutoka, ameacha kutapika, lakini bado hatujajiridhisha kama ugonjwa alio nao ni Ebola maana yapo magonjwa mengine yanayoweza kumfanya awe na dalili hizo,” alisema.
Alisema mgonjwa huyo alipokelewa katika chumba maalum na kupelekwa katika wodi ya magonjwa hatari ambapo ametengwa na anaendelea vizuri. “Damu sasa imesimama kutoka, ameacha kutapika, lakini bado hatujajiridhisha kama ugonjwa alio nao ni Ebola maana yapo magonjwa mengine yanayoweza kumfanya awe na dalili hizo,” alisema.
Alisema dalili za awali za mgonjwa wa Ebola ni homa, uchovu wa viungo, mafua, koo kuwasha, kutapika na kuharisha.
No comments:
Post a Comment