Wa
kwanza ni injinia wa Airtel mkoani Iringa bw Joshua Kadege akitoa
ufafafanuzi kwa mwenyekiti wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo
la Isimani bw Anderson Mpululu jinsi mtambo wa mawasiliano uliowekwa na
Airtel kijiji hapo unavyofanya kazi ili kurahisisha mawasiliano katika
kijiji hicho.Airtel imeanza kufunga mitambo ya mawasiliano itakayotumia
nguvu za Nishati ya jua (solar) ili kufikisha mawasiliano katika maeneo
ya vijijini, kati ni meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania bw Jackson
Mmbando wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika kijijini Kimande
nje ya mji wa Iringa jana.
Kulia
ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando na bw Beda Kinunda
Meneja wa Mauzo wa airtel Mkoani Iringa wakiwa nje ya Mnara wa Airtel
unaotumia nguvu ya Nishati ya jua (solar) wakizungumza na
Mwenyekiti wa kijiji cha Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu
(shoto) mara baada ya Airtel kuzindua rasmi mnara wa mawasiliano
unaotumia nguvu za Solar katika kijiji cha Kimande tarafa ya
Pawaga-Jimbo la Isimani, Airtel imezindua mnara huo unaotumia nishati ya
jua kwa lengo la kufikisha mawasiliano katika maeneo ya vijiji ambapo
bado hakujafikiwa na umeme wa taifa
Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa kijiji
cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu
kuhakikisha wanaweka ulinzi shirikishi kulinda mtambo mpya wa
mawasiliano unaotumia nishati ya jua uliowekwa na Airtel ili
kufikisha huduma bora ya mawasiliano kijijini hapo, wakwanza kulia ni
Meneja Mauzo wa Airtel Nyanda za juu kusini Bw, Beda Kinunda na kushoto
ni Injinia wa Airtel mkoani Iringa bw Joshua Kadege. Hafla ya uzinduzi
ilifanyika kijijini Kimande nje ya mji wa Iringa jana
Kulia
ni Injinia wa airtel mkoani Iringa akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti
wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson
Mpululu anaedadisi ili kupata ufafanuzi wa jinsi mnara wa Airtel
unaotumia Nishati ya jua (solar) unavyofanya kazi mara baada ya Airtel
kuzindua mnara huo kijijini hapo jana
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma zenye wigo
mpana zaidi imezindua minara yake inayotumia Umeme unao tumia nguvu za
nishati ya Jua katika kijiji cha kimande kata ya itunguru mkoani
Iringa. Uzinduzi huo ni moja kati ya mikakati ya Airtel kuhakikisha
inaendeleza mipango yake ya kupanua upatikanaji wa mawasiliano katika
maeneo mbalimbali nchini kirahisi, kupunguza gharama za uendeshaji na
kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika maeneo yenye minara yake
nchini.
Akiongea
wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande kata ya
Itunungu Tarafa ya Pawaga Iringa Vijijini Bw, Andason Mpululu
ameushukuuru uongozi wa Airtel kwa kuweza kukabili changamoto za
mawasiliano kijijini hapo na kuwa sehemu ya uboreshaji wa uendeshaji wa
biashara mbalimbali hasa za kilimo cha mpunga ambapo hapo awali
upatikanaji wa soko ulikuwa mgumu sana kutokana na kutokua na
mawasiliano thabiti kama ilivyo sasa.
“Kwa
kupitia Mtandao na huduma ya Airtel money huduma za kifedha
zimeboreshwa, zimekua karibu zaidi na kuwawezesha wafanyabiashara
kupokea malipo ya bidhaa zao kirahisi, kwa gharama nafuu na bila
usumbufu wowote. Nimatumaini yetu kuwa kwa kupitia umeme wa sola gharama
za mawasiliano ya simu za mkononi yataaendelea kupungua na kuboreshwa
zaidi na kuleta tija kwa wananchi hasa wenye kipato kidogo” alisema bwa
Mpululu
Naye
mkazi wa kata ya Itunungu bwana Jumanne Zuberi alisema “tunashukuru
sana serikali kuwawezesha wawekezaji kuwekeza katika sekta ya
mawasiliano na hivyo kufikiwa na mtandao wa Airtel. Hapo zamani
upatikanaji wa mawasiliano ulikuwa ni changamoto kubwa hivyo kuwafanya
wakazi wa kijiji hapa kutembea umbali mrefu kupata mawasiliano.
Tunashukuru kwa sasa huduma za simu kijini hapa zimeweza kuboresha
shughuli mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kuboresha usalama wa raia na
mali zetu”.
Akiongea
kwa niaba ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Meneja Uhusiano bw,
Jackson Mmbando alisema” nia yetu ni kubadili matumizi ya mafuta ya
diesel na generator kuendesha mitambo yetu ya mawasiliano na kutumia
umeme wa nishati ya jua ambao utasaidia katika kutunza mazingira na
kupunguza gharama za uendeshaji ambazo zitatuwezasha kutoa huduma kwa
ufanisi Zaidi na kwa gharama nafuu ili kuwafikia watanzania wengi zaidi
na kusogeza huduma mbambali za kijamii karibu na wananchi zikiwemo
huduma za Elimu, Afya na Mawasiliano. Kazi kubwa kwa wananchi nikulinda
huduma hizi na kuzitumia vizuri kwa shughuli za maendeleo vijijini”.
Mawasiliano
ndio chachu ya maendeleo hivyo tunaamini kwa kutumia umeme wa jua hata
gharama za uendeshaji zitapungua hivyo kuwezesha ktoa huduma zenye
viwango vya juu kwa gharama nafuu kwa watumiaji na wateja wa Airtel
nchini nzima aliongeza Mmbando”
Kampuni
ya Airtel katika kurahisisha mawasiliano nchini inaendelea kufunga
mitambo ya umeme wa sola katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya
Tanga, Sumbawanga, Kigoma na mikoa mengine mingi. Mpaka sasa Airtel
imefanikiwa kufunga mitambo minne inayotumia nguvu za jua katika mkoa wa
iringa Iringa vijijini.Mpaka sasa Airtel inaongoza kwa kutoa huduma
zenye wigo mpana na ina vijiji na miji 50
No comments:
Post a Comment