Saintfiet akisaini mkataba na Yanga Julai mwaka huu, kulia ni mwesigwa na kushoto ni Seif Ahmad 'Magari' |
Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA Mbelgiji
Tom Saintfiet amefukuzwa usiku huu, baada ya kutofautiana sera na uongozi wa
Yanga na sasa Fredy Felix Minziro, aliyekuwa Msaidizi wake, atakaimu nafasi
yake.
Habari zaidi,
kuhusu kufukuzwa kwa kocha huyo, Yanga itatoa taarifa rasmi kesho asubuhi saa
3:00, makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani.
Mapema leo
mchana, uongozi wa Yanga ya Dar es Salaam, ulitangaza kuisimamisha kazi
Sekretarieti nzima ya klabu, akiwemo Katibu Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari,
Louis Sendeu, kutokana na kile ilichoeleza utendaji usioridhisha.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Makamu
Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema kwamba maamuzi hayo yamefuatia kikao
cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika tangu saa 5:30 leo hadi saa 9:30.
Wengine
wanaokumbwa na panga hilo ni Masoud Saad, aliyekuwa Ofisa Utawala, Philip
Chifuka aliyekuwa Mhasibu na Hafidh Saleh aliyekuwa Meneja ambaye anahamishiwa
kwenye majukumu mengine.
“Tumesitisha
mikataba ya sekretarieti nzima, pia tumefanya marekebisho, tumemtoa Meneja wa
timu na muda si mrefu tutamtangaza Meneja mwingie pamoja na sekretarieti
mpya,”alisema Sanga.
Aidha, Sanga
alisema Kocha Mbelgiji, Tom Saintfieti anapewa onyo kali kwa kuzungumza ovyo na
vyombo vya habari.
“Tumekwishakutana
naye mara kadhaa kumpa utaratibu wa kuzungumza na vyombo vya habari, sasa tutamuandikia
barua ya kumkumbusha wajibu wake na kuzingatia wajibu wake, kutozungumza na
vyombo vya habari holela,”alisema.
Kwa ujumla
maamuzi haya yanakuja baada ya Yanga kuanza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, ikiambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili za awali, kutokana na
sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi
na Jumatano ikachapwa mabao 3-0 Morogoro Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Sasa beki wa
zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Lawrence Mwalusako
atakaimu nafasi ya Katibu wa klabu hiyo, kufuatia kusimamishwa kwa Celestine
Mwesigwa, wakati kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Sekilojo Johnson Chambua atakuwa
Meneja mpya wa klabu hiyo, akirithi mikoba ya Hafidh Saleh.
Habari
kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba viongozi hao wapya watatangazwa wakati
wowote kuanzia sasa kurithi nafasi za viongozi walioondolewa madarakani, kutokana
na kile kilichoelezwa utendaji usioridhisha.
Nafasi
nyingine za Mhasibu mpya, iliyoachwa wazi na Philip Chifuka itakuwa chini ya
dada mmoja, aliyetajwa kwa jina moja tu, Rose aliyekuwa akifanya kazi ofisi
hiyo kwa muda mrefu, wakati Msemaji wa klabu iliyoachwa wazi na Louis Sendeu,
inaelezwa atapewa mdogo wa mke wa Ridhiwani Kikwete, aliyehesabu kura za
Abdallah Bin Kleb katika uchaguzi mdogo wa klabu, Julai 14.
Saintfiet amefungwa
mechi mbili Yanga katika mechi 14 alizoiongoza timu hiyo tangu ajiunge nayo,
Julai mwaka huu, akirithi mikoba ya Mserbia, Kostadin Bozidar Papic.
Katika mechi
hizo, zimo sita za Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame,
ambazo aliiwezesha Yanga kutwaa taji, ikipoteza mechi moja tu dhidi ya Atletico
ya Burundi.
REKODI YA SAINTFIET YANGA
1.
Yanga
Vs JKT Ruvu (Kirafiki) 2-0
2.
Yanga
Vs Atletico (Burundi, Kagame) 0-2
3.
Yanga
Vs Waw Salam (Sudan, Kagame) 7-1
4.
Yanga
Vs APR (Rwanda, Kagame) 2-0
5.
Yanga
Vs Mafunzo (Z’bar, Kagame) 1-1 (5-3penalti)
6.
Yanga
Vs APR (Rwanda, Kagame) 1-0
7.
Yanga
Vs Azam (Kagame) 2-0
8.
Yanga
Vs African Lyon (Kirafiki) 4-0
9.
Yanga
Vs Rayon (Kirafiki, Rwanda) 2-0
10.
Yanga
Vs Polisi (Kirafiiki, Rwanda) 2-1
11.
Yanga
Vs Coastal Union (Kirafiki) 2-1
12.
Yanga
Vs Moro United (Kirafiki) 4-0
13.
Yanga
Vs Prisons (Ligi Kuu) 0-0
14.
Yanga
Vs Mtibwa (Ligi Kuu) 0-3source http://bongostaz.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment