Mufti wa Tanzania Sheikh Issah Bin Shaaban Simba.
Na Datus Boniface.
Wakati
kundi kubwa la waumini wanaodaiwa kuwa ni wa dini ya Kiislam wakipanga
kufanya maandamano makubwa kwa ajili ya kumwondoa kwa nguvu Mufti wa
Tanzania, Sheikh Issah Bin Shaaban Simba, jeshi la Polisi limesema
hakuna mwenye ubavu wa kufanya hivyo.
Pia,jeshi
la Polisi limesema hakuna mwenye ubavu huo siyo kwa kumng’oa Mufti
bali pia kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta) Dkt. Joyce
Ndalichako, kwani wamewekwa kwa taratibu na sheria.
Hivyo,
kuna taratibu na sheria maalum ambazo zinaweza kufuatwa kwa lengo la
kuwaondoa, lakini siyo kundi la waumini au wanasiasa.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova ameonya kuwa
kundi lolote la kidini au kisiasa lenye adha hiyo halitavumiliwa.
“Ni
lazima ifahamike wazi kuwa jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua
madhubuti za kisheria pale ambapo kundi lolote la kidini, la kisiasa au
taasisi itakapobainika kuhatarisha usalama wa Wananchi wasio na
hatia”alisema
Hata
hivyo Kamanda Kova amewahakikishia uongozi wa BAKWATA kuwa, jeshi la
Polisi lipo makini, hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa hivyo
litakabiliana kikamilifu na kundi dogo au kubwa litakalojaribu kuvamia
ofisi hiyo.
Aidha, amesema maandamano ambayo siyo rasmi ambayo hayana kibali ni marufuku kufanyika na kundi lolote la dini au kisiasa.
No comments:
Post a Comment