Wataalam
wenye thamana ya kushughulikia kuundwa kwa Benki ya Pamoja ya Nchi za
Afrika Mashariki ameendelea tena na mkutano wao mjini Kigali kujadili
mikakati ya uundwaji huo na taasisi nyingine katika ukanda huu.
Mchumi
Mkuu wa Benki ya Taifa ya Rwanda anayeiwakilisha Rwanda katika
majadiliano hayo Dkt. Frank Kigabo amesema katika mkutano huo mazungumzo
yatalenga katika mada zilizobaki akiahidi kuwa hadi mwishoni mwa
mkutano huo Jumamosi wiki hii ufumbuzi utapatikana.
Naye
Katibu Mkuu Msaidizi anayeshughulikia Mipango na Miundombinu katika
Sekretariet ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Enos Bukuku amesema
wananchi wa Afrika mashariki wanasubiri kwa hamu kujua nini
kutakachoamuliwa na mkutano huo.
No comments:
Post a Comment