MAHAKAMA
nchini Misri imewahukumu kifo magaidi 14 na wengine wanne kifungo cha
maisha jela kwa kosa la kushambulia jeshi na maafisa wa polisi katika
rasi ya Sinai.
Watu hao
ni wafuasi wa kundi moja la wanamgambo ambao wamepatikana na hatia ya
kuwaua maafisa watatu wa polisi, mwanajeshi mmoja na raia katika
mashambulizi yaliyofanywa mwezi Juni na Julai mwaka 2011.
Eneo la Sinai la Misri kwa muda mrefu limekuwa likikabiliwa na matatizo ya kiuslama.
Mwezi
Agosti mwaka huu jeshi la Misri lilianzisha operesheni kali ya
kuimarisha usalama kwenye eneo hilo baada ya watu wasiojulikana kuuwa
askari 16 wa mpakani wa Misri.
No comments:
Post a Comment