Minziro kulia akiwa Kocha wa Makipa Yanga, Mfaume Athumani |
Na Mahmoud Zubeiry
KAIMU
Kocha Mkuu wa Yanga, Freddy Felix Isaya Kataraiya Minziro amesema
kwamba hawezi kusema yuko tayari kuwa Kocha Mkuu wa kudumu wa klabu
hiyo, kwa sababu jukumu hilo anaona litakuwa zito kwake, kulingana na
uzito wa klabu yenyewe.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jana baada ya mechi dhidi ya JKT Ruvu, ambayo
aliiongoza Yanga kushinda 4-1, beki huyo wa zamani wa Yanga, alisema
kwamba hawezi kuanza kutamba anatosha kuwa kocha Mkuu baada ya ushindi
huo, kwa sababu ligi ni ndefu.
“Siwezi
kusema natosha kuwa Kocha Mkuu, kwa sababu mambo ya mpira leo
umeshinda, kesho kuna kufungwa, nachoweza kusema namshukuru Mungu tu kwa
ushindi huu,”alisema mtaalamu huyo wa zamani wa mipira ya mkato wa
ndizi ‘Banana chop’.
Akiuzungumzia
ushindi huo, Minziro alisema umetokana na ushirikiano baina yake na
wachezaji, kwani alipewa jukumu la kukaimu ukocha mkuu ghafla tu jana,
baada ya kufukuzwa kwa aliyekuwa bosi wake, Mbelgiji, Tom Saintfiet.
Aidha,
Minziro alisema kwamba ushindi huo umetokana na timu kutumia vema
nafasi ilizopata jana, tofauti na ilivyokuwa kwenye mechi mbili
zilizopita, dhidi ya Prisons mjini Mbeya waliyotoka sare ya bila
kufungana na Mtibwa Sugar waliyofungwa 3-0 Morogoro.
Alisema
pia hali nzuri ya Uwanja wa Taifa, tofauti na wa Sokoine mjini Mbeya na
Jamhuri, Morogoro nayo ilichangia ushindi wa jana.
Kuelekea
mechi na watani wa jadi, Simba SC,Oktoba 3, mwaka huu, Minziro maarufu
kwa jina la utani Majeshi, alisema kwamba itakuwa ngumu, lakini kwa kuwa
hii si mara yak wake kuachiwa timu, atakabiliana na jukumu hilo.
Yanga
jana ilipata ushindi wa kwanza ndani ya mechi tatu za Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 4-1 kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hadi
mapumziko Yanga walikuwa tayari mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani
na Nahodha, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ dakika ya nne na Didier
Kavumbangu dakika ya 31, mabao yote yakitokana na kazi nzuri ya kiungo
mshambuliaji Simon Msuva.
Bao
la kwanza ulikuwa mpira wa adhabu uliopigwa na Haruna Niyonzima, baada
ya Msuva kuangushwa karibu kabisa na eneo la hatari la JKT Ruvu na bao
la pili dogo huyo aliyesajiliwa kutoka Moro United iliyoshuka daraja,
alimpa pasi mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Kavumbangu.
Kipindi
cha pili, Yanga walirudi tena kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la tatu
dakika ya 52, mfungaji Simon Msuva kabla ya Didier Kavumbangu kufunga
la nne dakika ya 65.
JKT ilipata bao lake la kufutia machozi dakika ya 68 mfungaji Credo Mwaipopo.
Katika
mchezo wa leo, Yanga ilicheza vizuri, wachezaji wakionana kwa pasi
nzuri ndefu na fupi, tofauti na ilivyokuwa kwenye iliyopita mjini
Morogoro, ambako walifungwa 3-0 na Mtibwa Sugar.
Ikumbukwe mechi ya kwanza, Yanga ililazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons mjini Mbeya.
Yanga
leo ilicheza chini ya kocha Msaidizi, Freddy Felix Minziro, baada ya
aliyekuwa Kocha Mkuu, Mbelgiji Tom Saintfiet kusitishiwa mkataba jana
usiku, kufuatia kutofautiana na uongozi.
Kikosi cha Yanga jana kilikuwa; Yaw
Berko, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin
Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan/Shamte Ally, Haruna
Niyonzima, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete, Hamisi Kiiza na Simon Msuva.
SOURCE http://bongostaz.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment