Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton amemtetea vikali mgombea urais wa chama cha Democrats nchini Marekani Barack Obama.
Katika
hotuba iliyochukua muda wa dakika 50 katika kongamano la chama hicho
linalofanyika mjini Charlotte, North Carolina, Clinton alikosoa sera za
uchumi za chama pinzani cha Republican.
Rais
Obama atamenyana na mgombea wa chama cha Republican Mitt Romney katika
uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Novemba.Bill alisisitiza kuwa sera ya
uchumi ya Barack Obama imeweza kuimarisha uchumi wa nchi hiyo ambao
ulikuwa umedorora. Bwana Clinton alimaliza hotuba yake kwa kumteua rais
Obama kuwa mgombea rasmi wa urais wa chama.
Hotuba
ya Clinton ni dalili ya kuimarika kwa uhusiano kati yake na Obama na
pia kama juhudi za kupiga jeki mvuto wa obama miongoni mwa wazungu
wanaofanya kazi.
Kura
za maoni zinaonyesha kuwa wapiga kura wa chama hicho wamekuwa
waangalifu sana kuhusu sera za Obama lakini Clinton ana rekodi nzuri ya
kuwashawishi watu kumuunga mkono Obama.
Clinton
aliambia wafuasi wa chama '' Amueni nchi mnayotaka kuishi. Ikiwa
mnataka viongozi wasio wajali basi pigieni kura chama cha Republican.
Mkitaka nchi yenye nafasi nyingi na ambayo majukumu yanagawanywa, basi
sote tuko pamoja. Lazima mumpigie kura Barack Obama na makamu wake Joe
Biden."
Bwana
Clinton alikosoa vikali chama cha republican kwa kuzuia juhudi za
uchepuzi wa uchumi na badala yake kujihusisha na mijadala kuhusu sera.
Kura
za maoni zinaonyesha Barack Obama akiongoza kwa asilimia 47 huku
mpinzani wake Mit Romney akimfuata kwa asilimia arobaini na sita.
No comments:
Post a Comment