
Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud
Bunge la Somalia limemchagua Hassan Sheikh Mohamud kuwa Rais mpya wa nchi hiyo.
Kulikuwa na wagombea 22 kwenye uchaguzi huo, akiwemo Rais anayeondoka Shariff Sheikh Ahmed na waziri mkuu Abdiweli Mohamed Ali.
Katika
raundi ya kwanza Sheikh Ahmed alikuwa amepata ushindi mwembamba wa kura
64 dhidi ya 60 alizopata Sheikh Mohamud.Hassan Sheikh Mohamud alishinda
kufuatia duru ya tatu ya upigaji kura, ambapo alikuwa anachuana na Rais
anayeondoka Shariff Sheikh Ahmed.
Kwa jumla wabunge 271 walipiga kura.
Katika
duru ya mwisho wabunge wengi waliowaunga mkono wagombea waliochujwa
walimuunga mkono Sheikh Mohamud , akapata kura 190 dhidi ya 70 alizopata
Rais anayeondoka.
Hii ni
mara ya kwanza kwa uchaguzi wa Rais kufanyika katika mji mkuu wa Somalia
Mogadishu, tangu kuondolewa kwa serikali ya kijeshi mwaka 1991.

No comments:
Post a Comment