Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, September 18, 2012

Spika Makinda Ashiriki Msiba Wa Baba Yake Mhe. Tundu Lissu



  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimfariji Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu alipofika kuhani msiba wa Marehemu baba yake Mhe. Tundu Lissu mzee Agustinio Lissu Mughwai Nyumbani kwake tegeta, Dar es Salaam. Mzee Lissu alifariki Jumapili tarehe 16 Septemba, 2012,endelea kupitia audiface jackson blogspot kwa habari zaidi..katika Hospitali ya Muhimbili, Dar es salaam na anatarajiwa kuzikwa jumamosi Singida. 
 Mhe. Spika akimsalimia msemaji wa familia Ndg. Boniface Lissu 
 Spika wa Bunge akisaini kitabu cha maombolezo katika msiba wa baba yake Mhe. Tundu Lissu Mzee Agustinio Lissu Mughwai alipofika kuhani msiba huo Tegeta Dar es salaam
 Mhe. Spika akimfariji mbunge wa Viti maalum Chadema Mhe. Christina Lissu ambaye pia ni dada yake na Mhe. Tundu Lissu alipowatembelea kuhani msiba wa baba yao Tegeta, Dar es Salaam
Mbunge wa Singida Mjini Mhe. Tundu Lissu akiteta jambo na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda alipofika kuhani msiba wa baba yake Mhe. Lissu Mzee Agustinio Lissu Mughwai Tegeta Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment