Msanii wa kizazi kipya Easy Business
ambaye ni maarufu kwa kibao chake cha “Ongea na Mshua” akitumbuiza
katika mpabano wa STR8MUZIK 2012 FreeStyle Mwanza.
|
Mashabiki wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani Mwanza wakiwa wamembeba juu MC bora wa mwaka mkoani humo Joash Magadula katika mpambano uliofanyika jana usiku katika ukumbi wa Stone mjini humo. |
Umati wa wana-Mwanza ulivyoshona katika ukumbi Club Stone mjini humo katika mpambano wa STR8MUZIK 2012 FreeStyle Mwanza. |
Meneja wa TCC Mkoani Mwanza Deogratius Kamugisha akimkabidhi tuzo MC bora wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani Mwanza Joash Magadula katika mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Stone mjini humo jana. |
*****************************************
Na Mwandishi wetu Mwanza
FAINALI za tamasha la muziki la STR8 zilimalizika jana mjini hapa kwa kishindo cha aina yake huku tuzo ya DJ bora yenye thamani ya thamani ya sh milioni saba ikimuangukia DJ Juma Ramadhani.
Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika wakati ma DJs na Ma MCs wakipambana vikali kuwania moja ya kifaa cha kisasa kabisa katika masuala ya kuchezesha muziki, DJ Pioneer.
Ruyobya Johaness a.k.a DJ YT alikamata nafasi ya pili katika kategori ya MCs akiondoka zawadi kadhaa zikiwemo fedha taslimu 100,000/= .
Mshindi katika kategori ya MC alikuwa ni Joash Magadula ambaye pamoja na tuzo pia amepata nafasi ya kurekodi albamu katika moja ya studio tatu bomba za muziki nchini.
Nchana Anthony, alishika nafasi ya pili katika kategori hiyo ya ma-MC aliondoka nyumbani na zawadi kadhaa na fedha taslimu 100,000/=.
Fainali hizo ambazo ni za tatu tangu zianzishwe nchini zinaratibiwa na kampuni ya Sigara nchini (TCC) kwa lengo la kukuza vipaji miongoni mwa vijana na kutengeneza nafasi ya ajira.
Michuano hiyo ambayo ilikuwa na maMc 85 na Madj 25 zilichuja washindani wake hadi 16 kwa MC na 10 kwa maDJ katika raundi ya kwanza kabla ya raundi ya pili kutoa washiriki wa fainali.
Wakati MaDJ wakichukua nafasi zao katika tamasha hilo wapenzi wa burudani hawakuwa na la kufanya zaidi ya kuondoka na staili zao huku wakiwafagilia au kuwazodoa hivyo kuwapanga kimtindo katika nafasi za ushindani .
MaDJ hao walipewa maksi kwa kuangaliwa na majaji kuhusu uwezo wao wa kuchanganya muziki, uwezo wa kiufundi na wanavyomudu vifaa wanavyofanyiakazi na jinsi wanavyoburudisha.
Ma DJ sita waliofika fainali walikuwa Bernard Fabian, DJ Yt, Robert Rowan, DJ Megastar, Tony Wyclif na Juma Ramadhani.
Kategori ya MC ilihusisha DJ kupewa mada ya kukieleza kwa mtindo wa kufoka foka kwa dakika tatu kiushairi kimpangilio.
Raundi ya kwanza ya kategori hiyo ilihusisha MCs wote kisha ikawapunguza kwa pea hali ambayo ilifanya fainali hizo kuwa burudani babu kubwa hasa kutokana na jinsi wahusika walivyowachambua wenzao.
Matukio hayo ya fainali yalinogeshwa na burudani mbalimbali zikiwamo zilizotolewa na wakali wa Bongo Fleva kama Easy Business ambaye anajulikana kitaani kwa wimbo wake wa ‘Ridhiwani Ongea na Mshua’ .
Pia walikuwapo vijana wa kundi la Mwanza la BFB ambapo madansa wake walivamia jukwaa kwa staili huru zilizowapeleka puta wapenzi wa burudani waliokuwapo hapo.Madansa hao waliondoka kwa mitindo tofauti ikiwamo ya sarakasi na pop.
Aliyetingisha zaidi katika vionjo ni yule aliyetwaa ushindi mwaka 2010 katika kategori ya MCs, DJ Simba, ambaye alionesha ubabe wake katika kucheza na biti kiasi cha kufanya ukumbi mzima kurindima kwa shangwe.
Katika kategori ya MCs majaji waliangalia uwezo wa washiriki katika kumiliki maikrofoni,ufundi wake, uhalisia na staili.
Kwa mujibu wa waratibu wa michuano hiyo, ilikuwa taabu kubwa kumpata mshindi kutokana na wahusika kuwa wakali katika nafasi zao hali inayodhirisha utajiri wa vipaji vya muziki miongoni mwa vijana.
“Viopaji hivi vinatakiwa kulelewa na kuendelezwa,” alisema Deogratius Kamugisha, mwenyeji wa mashindano haya ambaye pia ni Meneja wa TCC Mwanza.
Alisema kwamba michuano hiyo ilikuwa si tu burudani bali pia ilitoa mwanya wa mafanikio mengine kama ajira.
Alisema washindi wa michuano iliyopita kwa sasa wako katika ajira mbalimbali zikiwemo vilabu vya usiku na vituo vya radio.
Kamugisha aliongeza: ” Hii ni namna ya kutengeneza ajira” alisema na kuongeza kwamba mashine ya kuchezea muziki kama aliyopewa Juma Ramadhani ni chanzo cha ajira kwani anaweza kuitumia yeye au kuikodisha kwa wengine anapokuwa hana kazi nayo.
Mchuano mingine miwili itafanyika mjini Dar es Salaam na Mbeya kukamilisha tamasha la mwaka huu.(Picha zote na Executive Solutions)

No comments:
Post a Comment