Msajili
wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia
mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia
usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa
amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na
wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.
Katika
hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyakati za uchaguzi
ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu
vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.
Source:Habari Radio Tumaini.
No comments:
Post a Comment