Mjumbe
wa jukwaa la wahariri kutoka Zanzibar Masoud Sanani kwenye maandamano
hayo Jangwani alitangaza maazimio yaliyofikiwa na washiriki wa
maandamano hayo, namkariri akisema “kwa siku 40 hizi za maombolezo
tusiandike habari ya polisi, polisi hata akifanya kitu gani tusiandike,
wataandika kwenye gazeti lao la polisi wanalo”
Katibu
wa jukwaa la wahariri Tanzania Neville Meena alizungumza pia na
kuamplfy kwamba vyombo vya habari vinafanya kazi kubwa kwa kufuata
taaluma na havipo kwa ajili ya maslahi ya mtu yoyote.
Namkariri
akisema “sheria zetu ni kandamizi sana ndio maana leo hii tunahangaika,
Wakuu wa Polisi Iringa na wenzie waliohusika na lile jambo ambao
ushahidi uonyesha kabisa kwamba kuna kuhusika kwa polisi wamekaa kimya
mpaka leo, hatujasikia polisi wanasema jambo lolote mpaka leo, kwa
sababu sheria zetu zimekaa vibaya kwa hiyo jitihada za kuhakikisha
tunapata sheria mpya za habari tuendelee nazo tupate sheria mpya ili
mwisho wa siku tuhakikishe tunakua na maisha salama”Baada
ya hapo sauti kupitia kipaza sauti ilisikika ikisema “kwa sababu
mmesema, tukampelekea ujumbe Mh Waziri hawa jamaa wanasema tupishe,
tunakuomba gari yako iko pale taratibu tunaomba uondoke, amewaona
akaamua aondoke… hatuna ugomvi na serikali wala hatuna ugomvi na wizara
yoyote ile ila shughuli ya leo imemkataa na tunaomba salamu zetu
zimfikie kwamba tunampenda sana, ni rafiki yetu ni Kwenye
line nyingine ni kwamba waandishi hao wa habari walioandamana
walilazimika kupinga ujio wa Waziri wa mambo ya ndani Dr Emmanuel
Nchimbi aliehudhuria maandamano hayo Jangwani ambapo waandishi
walisikika wakisema “maandamano haya ni ya waandishi na wahariri wetu
kwa hiyo Nchimbi aondoke
No comments:
Post a Comment