Mtibwa wakitoka uwanjani kifua mbele |
Wababe wa Yanga leo |
Yanga vibonde |
Jamal Bayser, Mratibu wa Mtibwa Sugar akifuatilia mechi |
Mabosin wa Yanga hoi |
Edibily Lunyamila akifuatilia mchezo |
Majjid hoi |
Na Mahmoud Zubeiry,
Morogoro
YANGA SC ya
Dar es Salaam leo imechapwa mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro kwenye Uwanja
wa Jamhuri mjini hapa.
Hadi
mapumziko, tayari Mtibwa Sugar walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani
na beki wa kati, Dickson Daudi dakika ya 11 akiunganisha kwa kichwa kona ya
beki wa kushoto Malika Ndeule.
Bao hilo
lilitokana na uzembe wa mabeki wa Yanga ambao walishindwa kumuweka ulinzi
mchezaji mrefu kuliko wote, Daudi.
Yanga
walijaribu kutaka kusawazisha, lakini mipango yao ilikuwa hafifu na kujikuta
wakiendelea kushambuliwa na dakika ya 43, Hussein Javu aliwainua tena vitini
mashabiki wa Simba waliokuwa wakiwashangilia kwa nguvu leo kwa kufunga bao la
pili.
Kwa ujumla
kipindi cha kwanza, Yanga walicheza ovyo- pasi zao nyingi zilikuwa hazifiki,
walishindwa kuwabana wapinzani wao na zaidi Haruna Niyonzima alishindwa
kuiongoza vema timu, jambo ambalo lilifamnya kiungo mkabaji Athumani Iddi
‘Chuji’ kupanda mbele zaidi kusaidia, ingawa haikusaidia.
Mabeki
wawili wa kati wa Mtibwa, Daudi na Salvatory Ntebe waliwadhibiti vema washambuliaji
wawili wa Yanga, Hamisi Kiiza na Saidi Bahamnuzi katika dakika 45 za kipindi
cha kwanza.
Kipindi cha
pili, Kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet alianza kwa mabadiliko akiwatoa
Frank Damayo na David Luhende na kuwaingiza Simon Msuva na Stefano na Mwasyika,
lakini bado ukuta wa Mtibwa ulikuwa mgumu mbele ya Watoto wa Jangwani.
Katika
kuongeza mashambulizi, Mtakatifu Tom alimtoa beki Mbuyu Twite na kumuingiza na
mshambuliaji Didier Kavumbangu, lakini bado mambo yaliendelea kuwa magumu kwa
Yanga.
Dakika ya 86
Hussein Javu aliifungia Mtibwa bao la tatu kwa shuti la mbali, wakitoka
kushambuliwa na kufikia hapo, Yanga ‘walikufa’ na mashabiki wao wakaanza
kuuacha Uwanja wa Jamhuri.
Huu unakuwa
mchezo wa pili kwa Yanga tangu kuanza kwa ligi wakiwasononesha mashabiki wao,
baada ya mechi ya kwanza kulazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye
Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Waswahili
wanasema siku ya kufa nyani, miti yote huteleza, Hamisi Kiiza alipaisha mkwaju
wa penalti dakika ya 89, baada ya Daudi kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, ,
Mbuyu Twite/Kavumbangu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi
‘Chuji’, Frank Domayo/Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi
Kiiza na David Luhende/Stefano Mwasyika.
Mtibwa Sugar; Shaaban Hassan Kado, Malika Ndeule, Issa
R Issa, Dickson Daudi, Salvatory Ntebe, Shaaban Nditi, Jamal Mnyate/Babu Seif Ally, Awadh
Juma, Hussein Javu, Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Vincent Barnabas/Ally Mohamed 'Gaucho'.SOURCE http://bongostaz.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment