Mwishoni mwa wiki iliyopita, kulikuwa na
taarifa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Patrick L. Tsere
amepewa barua na Serikali ya Malawi inayomtaka kuondoka nchini humo
ndani ya saa 48 kutokana na maoni yanayohusiana na mipaka ya Ziwa
Nyasa/Malawi aliyoyatoa redioni alipokuwa akizungumza katika mahojiano
na kipindi kimoja cha redio ya Zodiac ya nchini humo.
BBC Swahili katika kipindi chake cha Dira kimerusha mahojiano yake na Balozi Tsere kuhusiana na taarifa hiyo.
Balozi amesema aliyetoa chapisho hilo amekamatwa na Polisi wa nchini Malawi, ingawaje huo siyo uthibitisho kuwa kukamatwa kwake kunatokana na chapisho husika lililotoa uvumi ambao umekanushwa pia na Serikali ya Malawi.
No comments:
Post a Comment