Azam FC |
AZAM FC
tayari wapo mjini Mbeya tangu jana saa 1:00 usiku, kwa ajili ya yao ya
Jumatano, dhidi ya wenyeji Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini humo.
Azam
waliondoka Morogoro jana asubuhi baada ya mechi yao ya juzi dhidi ya Polisi
kwenye Uwanja wa Jamhuri na watafanya mazoezi kuanzia leo, ili kuzoea hali ya
hewa ya mji huo.
Mbeya ni
kati ya vituo ambavyo vinawaogopesha vigogo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, Azam, Simba na Yanga kutokana na imani kwamba Prisons haifungiki kwenye
Uwanja wake.
Sababu kubwa
ni ubovu wa Uwanja wa Sokoine, ambao wenyewe Prisons wameuzoea na wanaujulia,
wakati timu nyingine hupata tabu mno.
Kati ya
vigogo hao watatu, ambao wanafukuzana kuwania ubingwa wa Ligi Kuu, Azam inakuwa
timu ya pili kwenda Mbeya, baada ya Yanga iliyolazimishwa sare ya bila kufungana
na Wajelajela hao kwenye mechi yao ya kwanza ya ligi hiyo.
Simba
imeanzia Dar es Salaam kucheza na Prisons, Septemba 29, mwaka huu katika mechi
ambayo walishinda kwa taabu mabao 2-1 na sasa watarudiana na Wajelajela hao
mjini Mbeya katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Mikoa
mingine tishio ni Kanda ya Ziwa, ambako Azam tayari imekwishamaliza na
kukusanya pointi nne baa ya kuifunga 1-0 Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba kabla
ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Yanga pia
imemaliza deni la Kanda ya Ziwa, ikiambulia pointi tatu, baada ya kufungwa 1-0
na Kagera na kushinda 3-1 dhidi ya Toto.
No comments:
Post a Comment