Mwanadiplomasia
wa zamani wa Libya Ali Zeidan (Pichani) amechaguliwa na Bunge la nchini
hiyo kuwa Waziri Mkuu mpya pamoja na kuwa anakabiliwa na changamoto
kubwa ya kuliteuwa baraza la mawaziri, ambalo litakubaliwa na vyama
vyote katika nchi hiyo.
Mtangulizi
wake, Mustafa Abushagur ameondolewa baada ya kura ya kutokuwa na imani
naye bungeni mwanzoni mwa mwezi huu, baada ya mawaziri aliowateua
kupingwa ndani na nje ya bunge hilo.
Libya
inahitaji haraka serikali ili kuweza kuikarabati nchi iliyoharibiwa na
vita na kuleta maridhiano miongoni mwa raia baada ya mgawanyiko
uliosababishwa na vita vya kumuondoa madarakani Kanali Muamar Gaddafi
No comments:
Post a Comment