Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, October 12, 2012

Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mr. Patrick Tsere AFUKUZWA




Tanzania patrick tsere malawi Saga la ziwa Nyasa; Malawi yamfukuza Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mr. Patrick Tsere
Balozi Patrick Tsere kwenye interview hiyo iliyuzua sakata la yeye kufukuzwa nchini Malawi. Picha kutoka zodiakmalawi.com

Kwa mujibu wa website ya MalawiVoice, Serikali ya Malawi imemfukuza balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mh. Patrick Tsere, na kumpa masaa 48 aondoke nchini humo. Ripoti zilizotoka ikulu ya
Malawi zinasema Mr. Tsere ametajwa kuwa ni person-non-grata, ambayo katika ulimwengu wa diplomasia, inamaanisha ni mgeni asiyekaribishwa, na serikali ya nchi hiyo imekata mawasiliano ya kidiplomasia na mwanadiplomasia huyo.

Hatua hii imefuatia mahojiano aliyofanyiwa Mr. Tsere na gazeti la Zodiak Malawi ambapo alitamka wazi kwamba nusu ya ziwa Nyasa baada ya mpaka wa Msumbiji, inamilikiwa na Tanzania.
“Hili sio ziwa Malawi. Ni ziwa Nyasa. Linamilikiwa na mataifa yote yanayolizunguka, Tanzania, Malawi na Msumbiji.” Alisema Mr. Tsere katika mahojiano hayo
Ripoti hiyo inasema Mr. Tsere amepewa masaa 48 aondoke Malawi. Malawi hivi karibuni imekua ikiishutumu Tanzania kupeleka wanajeshi kufanya doria kwenye upande wa ziwa ambao Tanzania inadai ni wakwake. Pia ripoti hiyo imelalamika kwamba askari hao wa Tanzania wamekua wakiwanyanyasa na kuwakamata wavuvi wa Malawi kwenye upande wa ziwa ambao Tanzania inadai ni wakwake.
Tukio hilo limekumbusha wakati rais wa Malawi aliyepita, hayati Bingu wa Mutharika alipomfukuza balozi wa Uingereza nchini Malawi.

No comments:

Post a Comment