Meneja
wa Bia ya Safari Lager, Kabula Nshimo (kushoto) akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu washindi bora 6 waliofuzu katika shindano la shabiki
bomba wa Superfans Dar es Salaam
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Kabula Nshimo akiwa na baadhi ya washindi wakiwa na t-shirt za Castle Lager
Mmoja wa walioingia sita bora kutoka Iringa, Denis Mlowe
John Mosha kutoka Dar es Salaam
Yahya Hamza kutoka Mwanza
Filberth Nestory kutoka Dar es Salaam
Steven Chuma kutoka Dar es Salaam
Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE
mashabiki sita wakaochuana ili kupata wawili kupitia shindano la kusaka
mashabiki bora wa Ligi Kuu ya England, maarufu zaidi kwa jina la ‘Castle
Lager Superfans’, wamejulikana.
Washindi
hao sita wamepatikana kutokana na mchujo mkali kutoka kwa mashabiki 361
waliojitokeza kushiriki shindano hilo linaloendeshwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Castle Lager.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya
Castle Lager, Kabula Nshimo alisema ilikuwa ni mchujo mgumu, kutokana na
wingi wa mashabiki waliojitokeza.
Kabula
alisema, miongoni mwa hao sita, watapatikana wawili ambao ndio
watakaoungana na mashabiki kutoka nchi nyingine kuunda timu ya
ushangiliaji katika fainali za Kombe la Mataifa Afrika, zitakazofanyika
Afrika Kusini mwakani.
Aliwataja
mashabiki hao sita na mikoa wanayotoka ikiwa kwenye mabano kuwa ni,
Stephen Chuma , John Mosha, Filbert Nestory (Dar es Salaam), Charles
Mbaza (Arusha), Denis Mlowe (Iringa) na Yahaya Hamza (Mwanza).
Castle
Lager ambao pia ni wadhamini wenza wa Ligi Kuu ya England, itawatembeza
mashabiki hao mikoa yote ili kuomba kura, pia kupitia promosheni
mbalimbali zitakazoendeshwa nchi nzima.
Kabula
alisema, mashabiki 361 walijitokeza kwa kutuma picha zao katika mtandao
wa kijamii wa Facebook na promosheni walizoziendesha katika mikoa
mbalimbali.
Meneja
huyo alisema, baada ya mchujo walipatikana washindi 32 kutoka mikoa ya
Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Shinyanga, Mwanza, Arusha na Kilimanjaro,
ambao walipigiwa kura na kupatikana 15.
“Katika
hao 15 ndio ambao walifanyiwa mahojiano ya ana kwa ana, hivyo wamechujwa
na kupatikana sita, ambapo watasakwa washindi wawili ili waunde timu ya
Castle Lager Superfans Tanzania,” alisema.
Kabula
alisema washindi hao wawili watakaopatikana, wataungana na wengine
kutoka Swaziland, Zambia, Afrika Kusini na Zimbabwe ili kuunda timu ya
ushangiliaji itakayogharamiwa kila kitu katika fainali za Kombe la
Mataifa Afrika hapo mwakani. Fainali hizo zitafanyika Afrika Kusini.
Mashabiki hao sita unaweza kuwapigia kura kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno ukitaja jina la mshiriki kwenda namba 0683 536631.
No comments:
Post a Comment