*Asema inakabiliwa na ukame wa viongozi waliopikika kimaadili
* Hata kupata wagombea hutegemea 'iokoteze' walioshindwa michujo au chaguzi za CCM
* Asema kwa mtaji huo haiwezi kuwa chama chenye tija na hatma njema kwa taifa.
KATIBU
Mkuu wa CCM, Wilson Mukama amesema Chadema hakiwezi kuwa chama chenye
tija na hatma njema kwa taifa kutokana na kulazimika kuokoteza hata
wagombea wake kutokana na wanaoshindwa kwenye michujo au chaguzi ndani
ya CCM. Alisema, Chadema na vyama vingine vya upinzania hapa nchini,
vinazama katika hali hiyo, kutokana na kutokuwa na tanuru imara
linalowawezesha kutoa viongozi waliopikika kimaadili, kama ilivyo ndani
ya CCM. Amesema, Chadema wanaposema, kwamba kwa CCM kutowafukuza au
kuwanyima uongozi baadhi ya wana-CCM ni kuizika CCM, huko ni kulia
kinyume kwamba kwa kutofanya hivyo CCM imewakosesha watu ambao
wangehamia kwao hivyo chama chao kinakufa.
Mukama
alisema hayo jana wakati wa sherehe ya kuwapongeza wana-CCM Kata ya
Msasani kwa kukamilisha chaguzi zao ndani ya chama katika kata hiyo,
iliyofanyika kweny6e ukumbi wa Maisha Club, Msasani jijini Dar es
Salaam. Mukama alisema, CCM ni taasisi iliyojengwa katika misingi imara
na mshikamano wake ni kama ngumi inayoundwa na vidole vitano na
kitaendelea kuwa imara kwa sababu viongozi wake wanatokana na tanuru
lililowapika kimaadili wakapikika.
"CCM
bwana ni tasisi yenye viongozi wenye chimbuko la maadili, siyo kama
vyama vingine vinaongozwa na wenye vilabu vya usiku halafu eti navyo ni
vyama vya kuweza kuongoza nchi", alisema Mukama. Alisema kutokana na CCM
kuwa chama chenye chimbuko la maadili bora, ndiyo sababu kila
kinapofanya uchaguzi wa kupata viongozi wake huwa ni wa kihistoria kwa
kuwa anayepenya kuwa kiongozi huwa amepita kwenye tanuru la uchujwaji wa
hali ya juu.
"Juzijuzi
tulipokuwa tunateua majina ya wagombea, Kamati yetu ya maadili,
haikuacha kuchunguza hatua kwa hatua na kwa makini kama kila aliyeomba
uongozi anazo sifa bora na zinakidhi viwango vya kushinda anayetakiwa
kuondolewa yeye abaki, hivi ndivyo chama chenye misingi ya uadilifu ya
uongozi kinavyokuwa", alisema Mukama na kuongeza:- "Sasa hivi vyama
vingine vinaweza kufanya mchujo wa aina hii? thubutu.
Si
mlisikia juzi juzi mbunge mmoja alijaribu kuonyesha nia ya kutaka
uenyekiti wa Chama fulani, wee mliona alivyofurumushwa". Mukama alisema,
wanaosema CCM inakufa ni wavivu kufanya tathmini au wanasema hivyo
kudanganya watu na nafsi zao huku wenyewe wakiwa wanajua kwamba CCM ni
imara tena kwa vigezo.
"Hivi
jamani tujiulize na wao (wapinzani) wakitaka pia wajiulize chama chenye
mwelekeo wa kufa kinaweza kupata wagombea ambao ni Wazee, Vijana kina
baba na kina mama tena wengi wasomi kabisa waliobobea hadi ngazi za
uprofesa, wanaokanyagana kwa wingi kama tulivyoona wakiomba uongozi
katika nafasi mbalimbali? ", alihoji Mukama. Alisema, tutokana na hali
ya uchaguzi ndani ya Chama iliyojionyesha katika ngazi za mikoa, baada
ya kumalizika ngazi ya taifa, CCM itakuwa itakuwa imara zaidi tayari kwa
kutwaa dola tena baada ya uchaguzi mkuu wa 2015.
Katika
hafla hiyo, wanachama wa Kata hiyo, waliuopongeza uongozi wa juu wa CCM
kwa namna ulivyoweza kuweka taratibu zilizo wazi na za haki katika
kuhakikisha uchaguzi ndani ya chama unazaa viongozi walio dhabiti.
Mapema, Mukama alikabidhi hati kwa vijanan na makamanda wa Umoja wa
Vijana wa CCM, ambao wameshiriki katika shughuli mbali mbali za
kuimarisha chama kwa namna moja au nyingine.
No comments:
Post a Comment