CHAMA cha
Wananchi (CUF) kimekiri kuwabeba wafuasi wake kutoka jijini Dar es
Salaam ili kwenda kuhudhuria mkutano wao uliofanyika jijini Arusha
Jumapili iliyopita.
Wafuasi
hao waliletwa kwa mabasi kutoka wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke za
jijini Dar es Salaam pamoja na maeneo ya Tanga, Arumeru, Singida,
Handeni na Moshi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mipango, Uchaguzi na Siasa wa CUF, aliyasema hayo wakati
akitoa utambulisho juu ya viongozi waliohudhuria mkutano huo ambapo
alisema kuwa wilaya hizo mbali ya kuleta viongozi pia wameleta idadi
kubwa ya wanachama.
Tanzania
Daima ilishuhudia baadhi ya mabasi ya abiria aina ya Coaster
yaliyowaleta wanachama hao yakiwa yameegeshwa pembeni ya uwanja wa
mkutano, yenye namba za usajili T 941 CAK, T 992 BEK, T 393 AXY na T 477
BXA huku yakiwa yamefungwa bendera za chama hicho mbele na nyuma.
Pia
kulikuwa na magari aina ya Fuso ambayo hata hivyo namba zake za usajili
hazikuweza kufahamika mara moja kutokana na kuzibwa na bendera hizo
ambapo mara baada ya mkutano kumalizika, wananchi hao walitangaziwa kuwa
warudi kwenye magari yao tayari kwa ajili ya kuanza safari jana
asubuhi.
Mkutano
huo ulitawaliwa na shamrashamra za hapa na pale baada ya aliyekuwa
diwani wa CHADEMA Kata ya Elerai jijini Arusha, John Bayo, aliyefukuzwa
na chama chake, kutangaza kujiunga na CUF.
Mbele ya
Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, Katibu Mkuu, Maalim
Seif Sharif Hamad na viongozi wengine, Bayo alisema kuwa yeye aliwahi
kuwa mwanachama wa chama hicho mwaka 1992.
Alisema
kuwa alishiriki kutafuta wadhamini wa chama hicho kukiwezesha kupata
usajili wa kudumu, hivyo ameamua kurudi nyumbani baada ya kuchoshwa na
siasa za fujo.
Alisema
kuwa alisikitishwa na uamuzi wa Kamati Kuu ya CHADEMA yenye wajumbe 45
kumfukuza uanachama bila kuwauliza wananchi wake waliomchagua huku
akiendelea kulalamika kuwa hata waasisi wa CHADEMA walijaribu kutafuta
suluhu kwa kuwashauri madiwani hao kufuta kesi.
Maalim
Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alifika mkutanoni
hapo saa 3:46 alasiri akiwa na msafara wa magari ya serikali na ulinzi
mkali.
Akizungumza
na wananchi, Seif alisema kuwa chama hicho kilisinzia kuweka mizizi
mkoani Arusha licha ya kwamba mkoa huo una waasisi wengi wa CUF, hivyo
kuahidi kupiga kambi kwa ajili ya kukijenga upya.NA TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment