Wafuasi na wapenzi wa CUF wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad wakati akiwahutubia katika viwanja vya Buguruni jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wafuasi ya wapenzi wa
chama hicho katika viwanja vya Buguruni jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa ADC Bw. Al-Badawi akizungumza katika
mkutano wa hadhara wa CUF baada ya kuamua kurejea CUF akitokea ADC.
Kabla ya kwenda ADC na baadae kurejea CUF Al-Badawi alikuwa mwenyekiti
wa CUF Wilaya ya Temeke
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi shati la chama hicho
kijana Joseph Christian ambaye alikuwa katibu mwenezi wa CHADEMA tawi la
Chuo Kikuu Dodoma. Joseph amekihama CHADEMA na kujiunga na CUF kwenye
mkutano wa hadhara huko Buguruni jijini Dar es Salaam.Picha na Salmin
Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
---
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama
chake kitaendelea kutetea na kutekeleza sera yake ya kuwaunganisha
watanzania popote walipo bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Amesema
operesheni mchakamchaka hadi mwaka 2015 iliyozinduliwa na chama hicho
hivi karibuni imekuwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo,na kwamba
tayari imeanza kuleta mafanikio katika mikoa iliyoanza kutekelezwa
ukiwemo mkoa wa Arusha.
Maalim
Seif ametoa kauli hiyo katika viwanja vya Buguruni jijini Dar es Salaam
alipokuwa akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa chama hicho kwenye mkutano
maalum wa hadhara uliolenga kuwakaribisha wanachama wapya na kuwapokea
wanachama walioamua kurejea CUF baada ya kukihama na kuhamia vyama
vyengine.Katika mkutano huo Maalim Seif aliwapokea na kuwapa kadi za
chama hicho wanachama kadhaa walioamua kurejea chama hicho wakitokea
chama cha ADC wakiongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa ulinzi na usalama
wa ADC Bw.Al-Badawi.
Kabla
ya kujiunga na ADC, Bw. Al-Badawi alikuwa mwenyekiti wa CUF Wilaya ya
Temeke, na sasa ameamua kurejea CUF kwa kile alichokieleza kuwa ni
ubabaishaji ndani ya chama hicho kipya kinachohusishwa na mbunge wa
jimbo la Wawi Mhe. Hamad Rashid Mohd.
Maalim
Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema
Tanzania imekuwa ikipita katika kipindi kigumu cha migogoro na uvunjifu
wa amani, mambo ambayo yanapaswa kupigwa vita ili kurejesha hali ya
amani na kuvumiliana.
Amedai
kuwa chanzo kikuu cha migogoro ya kijamii ikiwemo ya ardhi na mizozo ya
kidini inatokana na kutokuwepo kwa mikakati imara ya kuendesha nchi, na
kwamba viongozi wanapaswa kujifunza kutokana na migogoro hiyo, ili
kuweka mikakati imara ya kuendesha nchi kwa uhakika.
“Nchi
haiendeshwi kwa kuigiza, bali kwa kuwa na viongozi wenye dira ya
mabadiliko kwa maendeleo ya wananchi”, alisisitiza Maalim Seif.
Amesema
kutokana na viongozi kutokuwa na dira na mikakati imara ya kuendesha
nchi, Watanzania wameshindwa kunufaika na rasilimali za nchi yao ambazo
ni nyingi na zinaweza kuwabadilisha kiuchumi.
Amefafanua
kuwa iwapo wananchi watanufaika moja kwa moja na rasilimali zao,
wataweza kuzitunza na kuzilinda ili ziwe endelevu, na kwamba kinyume
chake ni kuzihujumu rasilimali ambazo watahisi haziwanufaishi.
“Popote
pasipo na haki hakuna amani, tunataka kila Mtanzania ajihisi kuwa ana
haki sawa katika nchi hii, sio kuwa na raia wa madaraja, yaani daraja la
kwanza, la pili na latatu”,alifahamisha huku akishangaliwa na umati wa
watu waliojitokeza kwenye mkutano huo.
Katika
hatua nyengine, aliyekuwa katibu mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA katika tawi la Chuo Kikuu Dodoma bw. Joseph Christian
amejiengua katika chama hicho na kujiunga na CUF.
Akizungumza
katika mkutano huo bw. Joseph amesema ameamua kujiengua CHADEMA na
kujiunga na CUF kwa madai kuwa chama hicho kimekuwa kikiendeshwa kwa
misingi ya undugu na ukabila, na kuwatelekeza vijana wenye lengo la
kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini.
Amewatahadhamisha
vijana kuwa makini na sera za chama hicho na kuacha kukurupuka kuvamia
sera za vyama wasivyovifahamu.Nae Mwenyekiti wa ADC Wilaya ya Kinondoni
Bw. Saburi Mtoro, ambaye pia ameamua kukihama chama hicho na kujiunga na
CUF amemuahidi Katibu Mkuu wa CUF kuwa wanachama wote wa ADC katika
Wilaya hiyo watajiunga na CUF
No comments:
Post a Comment