Mama Beatrice Martin (pichani) mkazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani ambaye ana matatizo ya uvimbe mkubwa kwenye mguu wake wa Kulia kwa takribani miaka 15 uliyosababisha ashidwe kufanya shughuli yeyote ile ya maendeleo binafsi na akiwaomba watanzania waendelee kumsaidia kwa hali na mali ili aweze kujiunga na watanzania wenzake katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mama Martin anasema mpaka sasa ana kiasi cha shilling Millioni 8 benki na baada ya Mwandishi wa Habari kwa Kituo cha ITV kumkabidhi Million 4 sasa amefikisha Millioni 12 na ushee benki, kwa mujibu wa maelezo yake ameshawasiliana na madaktari wa hospitali ya Apollo nchini India na wamemhakikishia kwamba kuna uwezekano wa yeye kutibiwa bila kukatwa mguu lakini zinahitajika Millioni 27 fedha za kitanzania.
Kwa Mtanzania atakayetaka kuchangia kwa ajili ya matibabu ya mama huyu unaweza kutuma kupitia 0716- 850350 au 0767850351au account number 011201364730 NBC. 
Mkazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani, Bi Beatrice Martin akipokea pesa taslimu Millioni nne kutoka kwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha ITV Sam Mahela asubuhi leo, Baada ya Mwandishi huyo kufanya juhudi binafsi za kuchangisha fedha kwa watu mbalimbali ili kumsaidia mama huyo kwenda kupata matibabu nchini India. (Picha na Moblog).