KLABU ya Manchester United itaendelea
kuitangaza DHL katika jezi zao mazoezi, baada ya kukubaliana na kampuni
hiyo mkataba mpya wa udhamini wa jezi zao za mazoezi.
Wakati United inatangaza kuingia mkataba
wa awali na DHL mwaka 2010 wenye thamani ya pauni Milioni 40 kwa miaka
minne, ilikuwa ni kwa ajili ya maeneo yasiyo ya mkusanyiko wa watu na
mechi za kufuzu za Ligi ya Mabingwa.
Rio Ferdinand akiwa na jezi ya DHL mazoezini ambayo imelipa pauni Milioni 40 kudhamini
Tangu hapo, United imepiga hatua
nyingine kubwa ya kupata mkataba wa pauni Milioni 559 ya udhamini wa
jezi na kampuni ya General Motors, ambayo inavunja rekodi ya dunia kwa
kuchukua nafasi ya AON mwaka 2014.
Familia ya Glazer inayoimiliki klabu hiyo, imepiga hatua zaidi kwa kuinunua DHL, kuhakikisha wananufaika zaidi kwa mapato.
"Tumekamilisha vizuri mazungumzo ya
mkataba wa udhamini wa jezi za mazoezi na DHL, mara utakapomalizika tu
Juni 30, mwaka 2013," klabu hiyo ilithibitisha.
Familia ya Glazer
No comments:
Post a Comment