Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali kufuatia kubainika kwa matumizi ya dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi zenye jina la Biashara TT –VIR 30. Mmmoja wa maafisa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwenye vyombo vya habari akiwaonyesha waandishi wa habari Dawa badia za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVS) zilizoondolewa katika vituo vya kutolea huduma mara baada ya kugundulika. Makopo ya dawa za kupunguza makali ya Ukimwi yakitofautiana vifungashio. Kopo la kwanza kushoto linaonyesha dawa halisi ya kupunguza makali ya Ukimwi iliyokidhi viwango ikifuatiwa na makopo 3 yenye dawa bandia ya kupunguza makali ya Ukimwi yenye jina la biashara TT –VR 30 toleo namba 0c.01.85 yaliyotengenezwa na kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd.
Serikali
imewasimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD)
,Mkuu wa kitengo cha Udhibiti na Ubora na Afisa Udhibiti Ubora wa ohari
hiyo ili kupisha uchunguzi dhidi yao kufuatia kuruhusu kusambazwa kwa
dawa bandia za kupunguza makali ya UKIMWI aina ya TT –VIR 30 katika
vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya nchini.
Aidha
imepiga marufuku usambazaji na matumizi ya dawa aina ya TT –VIR 30
toleo na 0C .01.85 inayotengenezwa na kiwanda cha Tanzania
Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) kufuatia dawa hiyo kutengenezwa
chini ya kiwango na kutofaa kwa matumizi ya binadamu.
Akizungumza
leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein
Mwinyi amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa mara baada ya kubaini
kuwepo kwa dawa bandia ya kupunguza makali ya Ukimwi katika hospitali ya
wilaya ya Tarime kufuatia ukaguzi uliofanywa na Wizara ya Afya kupitia
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA).
Amesema
kuwa ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara dhidi ya dawa hiyo isiyokidhi
viwango ulibainia kuwa nyaraka zilizopo kuhusiana na dawa hizo
unaonyesha kuwa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI)
waliiuzia Bohari ya Dawa (MSD) dawa hiyo bandia toleo namba 0C. 01.
85 iliyotengenezwa nchini mwezi Machi 2011 na kuonyesha mwisho wa
matumizi yake mwezi Februari 2013.
Amefafanua kuwa
dawa hiyo bandia ilikua na dawa zenye rangi mbili tofauti njano na
nyeupe na kuwa na viambata tofauti vilivyopaswa kuwepo aina ya Efaverenz
badala ya Niverapine, Lamivudine na Stavudine na kuongeza kuwa vidonge
vilivyokutwa kwenye vifungashio vya dawa husika vilikua tofauti na
vifungashio vilivyosajiliwa na TFDA.
Dkt.
Mwinyi amesema kuwa serikali inahakikisha kuwa dawa zenye ubora
unaotakiwa za kupunguza makali ya UKIMWI zinaendelea kupatikana katika
vituo vya kutolea huduma kote nchini na kuwaagiza waganga wakuu wa
mikoa, wilaya na kamati za dawa na Tiba katika vituo vya huduma za afya
kuhakikisha kuwa zinapokea, kuhakiki na kusimamia kikamilifu ubora na
matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba nchini.
Kuhusu
upatikanaji wa dawa hizo amewatoa hofu wananchi na
kuwahakikishia kuwa dawa za kutosha zenye viwango stahili zitaendelea
kupatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini na kuwataka
wananchi kutoa kushirikiana na mamlaka husika kwa kutoa taarifa pale
wanapobaini kuwepo kwa dawa zenye ubora wenye mashaka au uvunjifu wa
sheria inayosimamia ubora na usalama wa dawa.
No comments:
Post a Comment