MLEZI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa mikoa ya Njombe,
Iringa na Mbeya, Thomas Nyimbo, ametangaza kujivua uanachama wa chama
hicho kwa madai ya kuchoshwa na siasa za ‘Umangimeza’ ndani ya vyama vya
siasa hapa nchini.
Nyimbo
ambaye amewahi kuwa mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka 10
katika Jimbo la Njombe Magharibi kabla ya kukimbilia Chadema mwaka 2010,
amesema hivi sasa atabaki kuwa mwanasiasa huru asiyefungamana na vyama.
Akitoa
taarifa ya kuachana na siasa ndani ya vyama jana, Jijini hapa, huku
akiwa ameambatana na mkewe Mary Mwenga, alisema amechukua uamuzi huo
baada ya kuona siasa za kushabikia vyama hazina tija kwa watanzania
walio wengi na badala yake zinawanufaisha viongozi wachahe
wanaojineemesha wao wenyewe kwa kutumia jasho la wananchi.
Akifafanua
zaidi alisema alichojiuzulu ni siasa za vyama, lakini sio siasa, huku
akitamba kuwa yeye alizaliwa akiwa ni mwanasiasa, kiongozi na mtu ambaye
mawazo yake yanahitajika kwa ajili ya maendeleo ya nchi yake, hivyo
atabaki kuwa mwanasiasa asiyekuwa na chama cha siasa.
Katika
taarifa hiyo aliyoitoa kwa vyombo vya habari mithiri ya Mhadhara,
Nyimbo alitumia zaidi ya saa moja na nusu kuelezea mustakabali wa taifa
na vijana kutokana na vyama vya siasa kuelekea kuwatumbukiza kwenye
machafuko.
“Nimeachana
na Chadema baada ya kubaini kuwa siasa za vyama havina tija kwa
wananchi na taifa kwa ujumla na ni wakati huu sasa wa kuachana na dhana
ya vyama vya siasa vituandalie sera na tunahitaji sasa itungwe sera ya
kitaifa ambayo mgombe inabidi atueleze tukimchagua ataitekeleza vipi”
alisema Nyimbo.
Alisema
hata nchi zenye wigo mpana wa Demokrasia kama Marekani ambao hivi sasa
wapo kwenye mchakato wa uchaguzi Mkuu huwezi kuwasikia wagombea wake
wakisifia vyama vyao, bali wanawaeleza wananchi wa Marekani watatekeleza
vipi sera ya nchi yao .
Alisema
kuwa ikiwa katiba mpya inayoandaliwa hivi sasa itakuruhusu mgombea
huru, atakuwa tayari kugombea ubunge tena kwenye jimbo lake la Njombe
Magharibi, lakini kama katiba hiyo itazuia fursa hiyo hatogomea tena
wadhifa huo maisha yake yote.
Aliongeza
kuwa baada ya kupatikana kwa katiba mpya, inabidi itungwe sera ya Taifa
itakayolindwa kisheria, ambayo kila chama kitakachofanikiwa kuingia
madarakani kilazimike kuifuata badala ya ilivyo sasa vyama vinaogelea
hovyo.
Alisema
kuwa ndoto za kuwa mwanasiasa huru alikuwa nazo tangu zamani, na ndiyo
sababu katika mabango yake ya kuhamasisha achaguliwe wakati akigombea
ubunge kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, alikuwa na kauli mbiu ya ‘Mtu
kwanza, chama baadaye.
Alisema
kuwa ikiwa katiba mpya inayoandaliwa hivi sasa itakuruhusu mgombea
huru, atakuwa tayari kugombea ubunge tena kwenye jimbo lake la Njombe
Magharibi, lakini kama katiba hiyo itazuia fursa hiyo hatogomea tena
wadhifa huo maisha yake yote.
“Nitapenda
kushauriana na watanzania wanaopenda maendeleo ya taifa letu nje ya
mlolongo wa vyama, hivyo hata kama naipenda vipi Chadema, nalazimika
kuresighn (kujiuzulu) uanachama ili niweze kutimiza azma hiyo,” alisema
Nyimbo.
Kilicho mkimbiza Chadema.
Alisema
ameamua kujiondoa ndani ya chama hicho baada ya kubaini kuwa kinaenda
kinyume na malengo yake kama kinavyojipambanua mbele za watu.
Alisema
licha ya kuwaaminisha wananchi, hususani vijana kuwa ndio chama chenye
kuleta mabadiliko ya kweli,lakini viongozi wake wa daraja la juu
akiwataja Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk. Wilbroad Slaa
wamekuwa wakijinufaisha binafsi.
Alisema
viongozi hao pia wamekuwa si watu wa kushaurika ndani ya chama hicho,
lakini kibaya zaidi ni kuendesha siasa katika mfumo mbaya wa kushawishi
na kuaminisha bila kuwa na suluhisho (Mob Politics).
Alisema
siasa za namna hiyo ni hatari kwa taifa kwa kuwa baada ya kuungwa mkono
kwa kiwango cha juu na kundi la vijana kwa imani ya kukombolewa pale
watakapofanikiwa kuingia madarakani na kushindwa kuwatimizia kutazua
vurugu.
Kuhusu CCM.
Nyimbo
alidai kuwa chama hicho kinajimaliza chenyewe kutokana na kuacha suala
la rushwa kwenye chaguzi zake za ndani kuwa ndio kigezo muhimu cha
kuwapata viongozi wake.
Hata
hivyo alisema ili tatizo hilo limalizike ni wananchi wenyewe kuamua
kuikataa rushwa kwa kupokea rushwa isiyoleta matunda kwani wakifanya
hivyo watakuwa wamemaliza tatizo hilo .
“Mfano
wewe ukipokea rushwa na kuamua kufanya tofauti na aliyekuhonga kwa kuwa
baadaye atakuwa hajapata kile alichotaka kukinunua toka kwako,
unafikiri kesho atarudia”.
Vijana.
Amewataka
vijana nchini kupigania maslahi yao kwa mtazamo hasi wenye kuleta
mstakabali mzuri wa Taifa, badala ya kufikiri kuwa mabadiliko ni
kuiondoa CCM madarakani na kuiweka Chadema.
Alisema
kuna mambo mengi ya msingi ambayo kama vinana wanapaswa kuwahoji
viongozi waliowachagua kama wameyatekeleeza , ikiwemo kupigania katiba
mpya kuwa na sera ya inayoweza kuruhusu mgombea binafsi kwa kuwa huko
wanaweza kupata viongozi bora.
Kujiengua
kwa Nyimbo linaweza kuwa ni pigo kubwa kwa Chadema, kwani baada ya
kujiunga na chama hicho mwaka 2010, alikuwa ni mlezi wa Chadema kwa
mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, huku pia akiwa ni miongoni mwa wanasiasa
wenye mvuto na wahamasishaji wazuri wa Chadema katika mkoa mpya wa
Njombe.
|
No comments:
Post a Comment