-YATAFANYIKA TAREHE 24-28 OKTOBA, 2012 JIJINI JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI
-KUSHIRIKISHA WABUNIFU ZAIDI YA 35 AFRIKA, NI MSHIRIKI PEKEE KUTOKA TANZANIA.
Mbunifu
maarufu wa mavazi kutoka Tanzania, Mustafa Hassanali ndiye Mtanzania
pekee katika fani ya mitindo aliyepewa mualiko wa kushiriki katika
maonyesho ya Wiki ya Mitindo Afrika chini ya African Fashion
International (AFI) yatakayofanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 24-28
Oktoba, 2012 katika ukumbi wa Melrose Arch, jijini Johannesburg, Afrika
ya Kusini.
Mashindano
hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya kutengeneza Magari ya Mercedes-Benz
yanatarajiwa kuwashirikisha wabunifu wa mavazi zaidi ya 35 kutoka sehemu
mbalimbali barani Afrika, baadhi ya nchi hizo ni wenyeji Afrika ya
Kusini, Ivory Coast, Morocco, Msumbiji, Cameroon, Rwanda, Angola, DRC,
Nigeria, Ghana na Tanzania.
“Ni
maonyesho ya pekee na yenye heshima yake barani Afrika na hata duniani
kwa ujumla kwani wabunifu walioalikwa ni wazoefu na bora katika fani ya
Mitindo barani Afrika. Hivyo mwaliko wangu si tu utaweza kutangaza kazi
ni nazofanya bali pia utasaidia kutangaza nchi yetu ya Tanzania kupitia
maonyesho haya” Alisema, Mustafa Hassanali.
“Watakapotaja
jina langu pale katika maonyesho, hawatasema tu huyu ni Mustafa
Hassanali, bali watasema huyu ni Mustafa Hassanali kutoka Tanzania,
hivyo itakuwa ni mchango mkubwa kwa nchi yetu kuweza kuonyesha fursa
zilizopo kupitia Ubunifu wa Mitindo. Nimejiandaa vizuri katika haya
maonyesho, nataka kuonyesha nini Tanzania tunacho katika tasnia ya
ubunifu kwa ulimwengu mzima ni imani yangu kufanya vizuri” Aliongeza
Hassanali.
AFI
inaandaa mashindano haya ili kuweza kutangaza kazi za wabunifu wa mavazi
kutoka barani Afrika katika soko la dunia kwani Afrika ina wabunifu
wazuri na imara hivyo kujitokeza kwao katika maonyesho haya kutafungua
milango zaidi katika soko la kimataifa na kuongeza fursa nyingi
zitakazoinua uchumi wa bara hili kupitia sanaa ya ubunifu wa mitindo.
Licha
ya kushiriki katika maonyesha haya, Mustafa Hassanali pia anawaomba
Watanzania wote kwa ujumla kuweza kumpigia kura ya kuwa mwanamitindo
bora barani Afrika kupitia tovuti yawww.awardnomination.afi.za.com na kuweza kuiletea sifa tasnia ya mitindo nchini Tanzania.
Huu
ni mwaka wa tisa kwa Mustafa Hassanali kupata mwaliko wa kuonyesha
ubunifu wake katika maonyesho haya. Ameshashiriki katika maonyesho zaidi
ya nchi 16 katika miji 25 tofauti duniani, amekuwepo katika kilinge cha
sanaa ya mitindo kwa muda mrefu hapa nchini, amechangia kwa kiasi
kikubwa mabadiliko na maendeleo ya kazi za ubunifu wa mavazi hapa
Tanzania.
No comments:
Post a Comment