Mtaalam
wa Mazingira wa UNDP Bw. Amani Ngusaro akitaja baadhi ya vikwazo vinavyo
kwamisha uboreshaji wa Mazingira katika maeneo ya makazi ikiwemo uhaba
wa maji na kutaka vikwazo hivyo viangaliwe upya na kuboreshwa sambamba
na kutolewa kwa elimu ya Mazingira na uhamasishaji katika ngazi zote.
Amefafanua
kuwa hata katika utekelezaji wa sera za serikali kama vile Kilimo
Kwanza elimu ya matumizi sahihi ya Ardhi inapaswa kutolewa kwa wakulima
ili utekelezaji wa sera hizo uwe na tija na ufanisi zaidi kwa manufaa ya
taifa.
Afisa
Misitu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Freddy Manyika akitoa
nasaha zake kwa kusema kuwa sisi wananchi ndio tunatakiwa kuwa wa kwanza
kufanya mabadiliko na sio kuilaumu serikali kwani ndio tunaozungukwa na
mazingira.
Aidha pia
ametumia nafasi hiyo kutangaza kuwa suala la mabadiliko ya hali ya hewa
sio jambo la mzaha hivyo serikali inatakiwa kuwa na sera madhubuti
zitakazo wawezesha wananchi kukabiliana na madhara yatokanayo na janga
hilo ili kujitahidi kuirejesha ardhi na mazingira yetu kwa ujumla katika
hali bora.
Mtaalamu
wa Ikolojia Profesa Raphael Mwaliosi akitoa mada wakati wa majadiliano
ya hadhara yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa ikiwa ni Sehemu ya
Maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja huo ambapo amechambua changamoto baina
ya Mazingira na Mabadiliko ya hali ya Hewa hapa nchini na jitihada za
kukabiliana nazo.
Ameongeza
kuwa changamoto zaidi zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa
zinaleta athari mpaka katika Nyanja ya kiuchumi akitolea mfano sekta za
Kilimo, Maji, Nishati, Afya, Misitu, Uvuvi na Utalii.
Pichani
Juu na Chini Wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali jijini wakitoa maoni
yao katika mjadala wa wazi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee ambapo
wamelalamikia baadhi ya Sera za Serikali zisizotekelezeka wakatu wa
maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa kusheherekea miaka 67.
Pichani
Juu na Chini ni Baadhi ya Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali jijini
waliohudhuria Mjadala wa wazi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa katika
kusheherekea miaka 67 tangu kuanzishwa.
No comments:
Post a Comment