Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Oljoro JKT ya Arusha
lililochezwa jana (Oktoba 7 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
kumalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 limeingiza sh.
46,680,000.
Watazamaji
8,081 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh.
5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo
wa sh. 8,172,396.61 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 7,120,677.97.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000,
kamishna wa mechi sh. 193,000, waamuzi sh. 210,000, mwamuzi wa akiba
(reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na
Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
Umeme
sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000,
ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 3,175,000. Gharama za
mchezo sh. 2,724,132.20, uwanja sh. 2,724,132.20, Kamati ya Ligi sh.
2,724,132.20, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
1,634,479.32 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,089,652.88.
No comments:
Post a Comment