Mkuu wa jeshi la polisi nchini mh Said Mwema
ASKARI
mwenye namba F 7961 PC Stanley Mdoe anayefanya katika kituo cha polisi
Mvomero Mkoani hapa anadaiwa kujihusisha na masuala ya siasa na kujikita
kwenye kinyang’anyiro cha kugombea ujumbe wa halmashauri kuu ya CCM
Taifa kupitia kundi la vijana.
Habari
zilizopatikana kutoka vyanzo vya habari zimedai kuwa askari huyo
anayejitambulisha kuwa yeye ni mtoto wa mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel
Bendera,akijitambulisha kwa jina la Stanley Bendera alikamatwa mkoani
Dodoma majira ya jioni uchaguzi wa umoja wa vija wa chama cha mapinduzi
ukiwa unaendelea.
Chanzo
hicho kilidai kuwa askari huyo akiwa amevalia sare za chama hicho tangu
siku ya kwanza huku akiomba kura kwa wajumbe ya kuchaguliwa kuwa MNEC
akiwa na wapambe wake ambao wengi wao walitokea mkoani Morogoro.
Ilidaiwa
kuwa askari huyo kwa mbwembwe akiwa amepamba gari yake kwa picha zake
zilizokuwa zimeandikwa Stanley Joel Bendera,baadahi ya wananchama wa
chama hicho wanaomfahamu waliwatonya maafisa usalama waliokuwepo eneo
hilo ambapo nao walitoa taarifa kwa jeshi la polisi mkoani Dodoma ndipo
alipotiwa mbaroni.
Aidha
askari huyo pamoja na juhudi zake za kusaka ujumbe wa NEC lakini
hakushinda uchaguzi huo na badala yake kujikuta akiangukia mikononi mwa
polisi.
Baadhi ya
vyanzo vya habari vilidai kuwa askari huyo tayari aliomba likizo
isiyokuwa na malipo na wengine kudai kuwa ameacha kazi,jambo
lililosukuma gazeti hili kumtafuta mwajiri wake kuzungumzia suala hilo.
Hata
hivyo gazeti hili baada ya kupata taarifa hizo ilimtafuta mwajiri wake
ambaye ni kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Faustine Shilogile ambaye
alisema kuwa hana taarifa ya askari huyo kujihusisha na masuala ya
kisiasa.
Shilogile
alisema kuwa alipata taarifa za kukamatwa kwa askari huyo mkoani humo
na kwamba yeye alikuwa akimtafuta kwa shughuli za kikazi kwa muda wa
siku mbiuli bila kumpata.
Aidha
kamanda huyo alisema hana uhakika kuwa askari huyo mejiingiza katika
siasa na kwa sasa ametuma askari wengine kwa ajili ya kwenda kufanya
uchunguzi wa suala hilo na endapo itabainika atachukuliwa hatua za
kinidhamu stahiki za jeshi hilo kulingana na taratibu za kijeshi.
“Kusema
kwamba aligombea siwezi kulizungumzia kwa kuwa sijadhibisha isipokuwa
hakuwepo kazini kwa siku mbili,huu ni utovu wa nidhamu kwa jeshi
letu,”alisema shilogile.
Alisema
kuhusu sheria,alisema katiba ya nchi sura ya 9 inayohusiana na majeshi
ya ulinzi kwa maana ya majeshi yote Tanzania inasema ni marufuku kwa
mwanajeshi yeyote kujihusisha na masuala ya siasa na kwamba kama ni
kweli amefanya hivyo ni kinyume,kanuni na taratibu za kazi.
No comments:
Post a Comment