Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Raphael Muhuga aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Tanzania katika sherehe za maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu kuzaliwa kwake Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta akiwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo katika Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa Tanzania kusheherekea miaka 67 tangu uanzishwe Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akimlaki na kumtambulisha kwa wakurugenzi wa UN Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaa leo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akizungumza katika sherehe za kutimiza miaka 67 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Sitta aliipongeza Umoja wa Mataifa kwa kuisaidia Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo ili kutokomeza umaskini.Waziri Sitta alisisitiza kwamba bado Umoja wa Mataifa unakabiliwa na changamoto nchini kama vile amani na usalama, tatizo la njaa, mabadiliko ya tabia nchi na uwepo wa silaha za maangamizi.Mh. Sitta alifafanua katika kilele cha sherehe hizo umuhimu wa kupitia na kusaidia nchi zinazoendelea kufikia malengo ya millennia
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akitoa nasaha zake
wakati wa maadhimisho ya umoja huo katika viwanja vya Karimjee alisema
matatizo ya njaa, kupanda kwa bei za mafuta na mtikisiko wa uchumi
duniani ni kati ya changamoto kubwa ambazo Umoja wa Mataifa inakabiliana
navyo katika dunia ya leo. Dtk Kacou pia aliipongeza Tanzania katika
juhudi zake za kupunguza vifo vya wakinamama wakati wa kujifungua na
watoto ili waweze kufikia malengo ya millennia itakapofika 2015.Mratibu
Mkazi wa UN alisema Tanzania imepunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi
mapya ya ugonjwa wa Ukimwi
No comments:
Post a Comment