Rais
Alpha Conde (pichani) wa Guinea amewafukuza kazi mawaziri 11 wa
serikali yake katika mabadiliko ya kushtukiza yaliyotangazwa Ijumaa
jioni na televisheni ya taifa.
Taarifa
kutoka ofisi ya rais haikubainisha sababu ya mabadiliko hayo, lakini
hatua hiyo imekuja wakati wasiwasi unaongezeka juu ya uchaguzi wa
wabunge uliyocheleweshwa.
Miongoni
mwa mabadiliko muhimu ni uteuzi wa Waziri Mkuu wa zamani na
mwanadiplomasia wa siku nyingi Francois Louceny Fall kuwa Waziri wa
Mambo ya Nje.
Katika
mabadiliko hayo Waziri wa Kilimo Jean Marc Telliano na Waziri wa Ujenzi
na Maendeleo ya miji Mathurin Bangura, ambaye anatuhumiwa kwa
kujilimbikizia mali akiwa mtumishi wa umma wamefukuzwa kazi.
No comments:
Post a Comment