Chelsea
imejiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya England, baada ya kuichapa mabao
4-1 Norwich nyumabni. Grant Holt aliifungia Norwich bao la kuongoza
dakika ya 11, lakini Chelsea ilisawazisha kupitia kwa Fernando Torres
kabla ya Frank Lapard na Eden Hazard kufunga mabao ya ushindi kipindi
hicho hicho cha kwanza na Branislav Ivanovic kuhitimisha karamu ya mabao
ya ushindi wa 4-1 zikiwa zimebaki dakika 15. Chelsea imefikisha pointi
19, baada ya kucheza mechi saba na kuendelea kuongoza Ligi Kuu,
ikiwazidi pointi nne mabingwa watetezi, Man City .

Eden Hazard akiifungia Chelsea

Fernando Torres akiwa chini ya ulinzi wa Javier Garrido na Leon Barnett

Torres baada ya kufunga

John Ruddy akitunguliwa na Frank Lampard

Frank Lampard baada ya kuifungia Chelsea

John Terry na Ashley Cole wote walicheza leo

Branislav Ivanovic akipongezwa na John Obi Mikel kwa kufunga bao la nne
No comments:
Post a Comment