Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki akiongea na waandishi wa
habari leo Ofisini kwake kuhusu kupinga maandamano wa Waislam
yaliyopangwa kufanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 02/11/2012 mara baada ya
swala
. MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM SAID MECK SADIKI ATOA TAMKO KALI KUHUSU MAANDAMANO YA WAISLAM YALIYOPANGWA KUFANYIKA SIKU YA IJUMAA MARA BAADA YA SWALA.
. MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM SAID MECK SADIKI ATOA TAMKO KALI KUHUSU MAANDAMANO YA WAISLAM YALIYOPANGWA KUFANYIKA SIKU YA IJUMAA MARA BAADA YA SWALA.
Na Adrophina Ndyeikiza-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam 31/11/2012.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki ametoa tamko kali la kuwataka Waislam kuacha mara moja kufanya maandamano yao yaliyopangwa kufanyika siku ya Ijuamaa ya tarehe 02/11/2012 mara baada ya swala ya Ijumaa.
Kwa
mujibu wa vipeperushi vilivyoandikwa na kusambazwa na Jumuiya na
Taasisi za Kiislam (Tz),vimewataka waislam kufanya maandamano makubwa
kuelekea katika Ofisi ya Mhe.Waziri Mkuu kwa upande wa Dar es Salaam na
Mikoani maandamano hayo yataelekea kwa wakuu wa Mikoa aidha kwa upande
wa Zanzibar yataelekea Ofisi ya Makamu wa Rais. Aidha,Sababu ya
kuandamana kwao wameelezea kuwa ni kushinikiza Serikali kutenda haki kwa
wananchi wote bila ubaguzi kwani waislam wanabaguliwa kwa mambo mengi
kama vile;- -Kudhalilishwa Masheikh wao kwa kukamatwa hovyo bila sababu
za msingi mfano,Sheikh Ponda na Sheikh Farid wakati wakristo
hawafanyiwi hivyo.
Akijibu hoja hiyo mbele ya waandishi wa habari
Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Sheikh Ponda hakukamatwa kama Sheikh Ponda
bali amekamatwa kama mtu yeyote yule ambaye anaweza kutuhumiwa kwa kosa
fulani.Ameongeza kuwa Serikali haikumkamata Sheikh Ponda kutokana
usheikh wake/dini yake au uislamu wake bali kutokana na kutuhumiwa
kwake.Hivyo tuache vyombo vya sheria vifanye kazi yake na haki
itazingatiwa tu.
“Alisisitiza Mkuu wa Mkoa”. -Sababu nyingine ni pamoja
na Kudhalilishwa matukufu ya Waislam huku Serikali ikikaa kimya.Akijibu
hoja hiyo pia Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema kuwa jambo hili si kweli kabisa
kwani Serikali ilikwishachukua hatua stahiki kwa kumkamata kijana huyo
aliyeyekojolea Koran na kumfikisha katika vyombo vya sheria,hivyo kijana
huyo alikwishakamatwa,hata hivyo wale wote waliokwenda kuchoma
makanisa,kupiga vioo vya magari ya watu na kuiba vitu mbalimbali katika
makanisa na ndani ya magari ya watu nao pia wapo katika mikono ya sheria
kwani uislam pia hauagizi hivyo.
Sababu ya tatu ni kuundiwa chombo cha
kusimamia Waislam kwa nia ya kuwadhibiti na kulazimishwa Waislam
kukitii pamoja na ukweli kwamba kinafisidi Uislam na Wislam.Akijibu hoja
hiyo Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema kuwa kamwe Serikali haiwezi kufanya
hivyo,kwani kila chombo kinaundwa na wanajamii husika na wala Serikali
haina dini hivyo haiwezi kuunda chombo chochote kile cha kidini.Hata
hivyo zipo taratibu maalumu za namna ya kusajili taasisi yoyote ile
kwani lazima kueleza mbele ya msajili ya kuwa taasisi yenu ni ipi na ina
malengo gani kwa jamii husika na msajili akilizika na maelezo yenu basi
huna budi kuisajili taasisi hiyo.Taasisi yoyote ile lazima isajiliwe na
ifuate taratibu za sheria,na Serikali inazisikiliza taasisi zote kama
zinafuata sheria na taratibu “Alisisitiza Mkuu wa Mkoa”.
Hivyo basi Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki amesema kuwa Waislam wote
wapenda amani wasifanye maandamano yoyote siku hiyo ya Ijumaa mara baada
ya swala kwani kwa kufanya hivyo HATUA KALI ZA KISHERIA DHIDI YA
WATAKAOHUSIKA KATIKA KUYAANDAA NA KUSHIRIKI ZITACHUKULIWA kwani
maandamano hayo ni BATILI na hayajaruhusiwa na JESHI LA POLISI. Sheria
kali zitachukuliwa katika suala hili “Alisisitiza Mkuu wa Mkoa”.
No comments:
Post a Comment