Juma Nyosso |
SIMBA
SC imekubali kuvunja mkataba na beki wake Juma Said Nyosso kulingana na
maombi yake, na imemtaka afike kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili,
Zacharia Hans Poppe kujadili suala hilo.
Habari
za ndani kutoka Simba SC, zimesema kwamba Nyosso amewasilisha maombi ya
kuvunja mkataba na klabu hiyo, baada ya kushushwa kikosi cha pili,
akidaiwa kiwango chake kimeshuka hivyo amepewa fursa ya kwenda
kukiboresha.
Lakini
Nyosso mwenyewe ameona kama hastahili kushushwa timu ya pili na ameomba
asitishiwe mkataba wake aondoke, jambo ambalo uongozi wa klabu
umelikubali.
Nyosso
si kama anatuhumiwa kuhujumu timu, bali anaambiwa uwezo wake umeshuka
mno na kwamba amekuwa akiigharimu timu katika siku za karibuni, hivyo
amepewa fursa ya kwenda kupandisha kiwango chake.
Adhabu
kama hii amewahi kupewa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Carlos
Tevez katika klabu ya Manchester City ya England msimu uliopita na
aliitumikia vizuri hadi aliporejeshwa tena kikosi cha kwanza, ambako
aliisaidia timu kumalizia msimu vizuri kwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu.
Mbali
na Nyosso, kiungo Haruna Moshi Shaaban amesimamishwa kwa wiki tatu kwa
tuhuma za utovu wa nidhamu na katika kipindi hicho atakuwa akipokea nusu
mshahara.
Boban
ameamua kurudi nyumbani kwake kupumzika na mkewe hadi adhabu hiyo iishe
ajue mustakabali wake, ila amesema anaonewa kwa sababu hakupewa nafasi
ya kujibu tuhuma zake kabla ya hatua kuchukuliwa, ingawa amechukulia poa
tu.
Wakati
huo huo, habari zaidi kutoka ndani ya Simba, zimesema kwamba Mwinyi
Kazimoto Mwitula, Ramadhan Suleiman Chombo na Mrisho Khalfan Ngassa nao
wanaangaliwa kwa ‘jicho la tatu’ juu ya mwenendo wao kwenye timu hiyo na
kwa nyakati tofauti wote wamekwishaitwa kuhojiwa masuala mbalimbali.
No comments:
Post a Comment