Na Habari Maelezo Zanzibar 24/10/2012
SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMEVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA
USALAMA NCHINI KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA ILI KUBAINI KIINI CHA
KUTOWEKA SHEIKH FARID HADI AHMED NA CHANZO CHA VURUGU ZILIZOTOKEA
NCHINI WIKI ILIYOPITA..
KWA MUJIBU WA TAARIFA ILIOTOLEWA NA WAZIRI WA NCHI AFISI YA MAKAMO WA PILI WA RAIS ZANZIBAR MH. MOHAMMED ABOUD AMESEMA
KUTOWEKA
KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA KWA SHEIKH FARID KULIPELEKEA KUZUKA KWA
MACHAFUKO KATIKA MAENEO KADHAA YA MJI WA ZANZIBAR AMBAPO MALI ZA WATU
ZILIPORWA NA KUHARIBU MIUNDO MBINU YA BARABARA NA KUCHOMA MOTO MASKANI
ZA CCM..
HIVYO
ILITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUFANYA TATHMINI ILI KUJUA KIWANGO
CHA HASARA KILICHOTOKANA NA VURUGU HIZO NA KUWACHUKULIA HATUA ZA
KISHERIA WALE WOTE WATAKAOBAINIKA KUHUSIKA NA KADHIA NZIMA YA SHEIKH
FARID,VURUGU NA MAUAJI YA ASKARI KOPLO SAID ABRAHMANI HUKO BUBUBU
WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.
AIDHA VYOMBO HIVYO VIMETAKIWA KUENDELEA NAKUDHIBITI HALI YA USALAMA WA NCHI KWA WAKATI WOTE KWA VILE VITENDO HIVYO
VIMEKUWA VIKIJITOKEZA MARA KWA MARA NA KUHAKIKISHA KWAMBA HAVIREJEI TENA.
TAARIFA
HIYO ILIENDELEA KUSISITIZA WANANCHI KUACHA VITENDO VYENYE KUHATARISHA
AMANI NA UTULIVU ULIOPO NCHINI KWA VILE CHUKI NA FUJO SIKU ZOTE KAZI
YAKE NI KUBOMOA NA SIO KUJENGA.
MH. ABOUD
ALIENDELEA KUSEMA KUWA WALE WOTE WENYE DHAMIRA YA
KUGOMBANISHA WANANACHI NA SERIKALI YAO NI VYEMA WAACHE KUFANYA HIVYO
BALI JAMBO LA MSINGI NI KUDUMISHA MASHIRIKIANO ILI KUJENGA NCHI YETU
KWA MASLAHI YA TAIFA NA VIZAZI VIJAVYO.
AMESEMA
KUWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INAWASHUKURU WANANCHI WOTE KWA
USTAHAMILIVU WAO NA PIA KUVISHUKURU VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KWA
KAZI NZURI WALIOIFANYA KUTULIZA FUJO NA VURUGU AMBAPO HIVI SASA HALI
IMEREJEA KUWA YA UTULIVU.
ALIONGEZA
KUWA HIVI SASA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VINAENDELEA KUDHIBITI HALI
HIYO NA KUWAOMBA WANANCHI WAENDELEE NA SHUGHULI ZAO ZA KAWAIDA BILA YA
WASIWASI.
KUHUSU
UCHUMI WANCHI, ALISEMA KUWA ADUI MKUBWA WA UCHUMI NI KWA NCHI KUINGIA
KATIKA VURUGU NA MACHAFUKO KUNAKOPELEKEA KUVUNJIKA KWA AMANI NA
UTULIVU AMBAPO ZANZIBAR UCHUMI WAKE MKUBWA NI KUTOKANA NA SEKATA MAMA
YA UTALII AMBAO HUATHIRIKA SANA KUKIKWA HAKUNA AMANI NA UTULIVU NA
KUREJESHA NYUMA MAENDELEO NA KUZIDISHA HALI YA UMASIKINI JAMBO AMBALO
HUONGEZA UPUNGUFU WA AJIRA KWA VIJANA WETU
WAZIRI HUYO AMEWASIHI WANANCHI WA ZANZIBAR HASA VIJANA KULINDA AMANI YA NCHI AMBAYO NDIO RASILMALI KUU YA TAIFA.
ALISEMA
KUWA PANAPOTOKEA TATIZO AU CHANGAMOTO YA AINA YOYOTE KWA MUJIBU WA
MISINGI YA UTAWALA BORA NA WAKIDEMOKRASIA NI BUSARA KUFANYIKA KWA
MAZUNGUMZO MIOUNGONI MWA WADAU WAHUSIKA.
TAARIFA
HIYO IMEONGEZA KUWA WAZANZIBARI WOTE NI NDUGU, NI WATU WAMOJA HAKUNA
BUDI KUPENDANA, KUAMINIANA, NA KUSAIDIANA KWA HIVYO VIACHWE VITENDO
VYENYE KUHATARISHA AMANI NA UTULIVU ULIOPO CHUKI NA FUJO HAZINA NAFASI
KATIA ULIMWENGU HUU, KWANI VITU HIVYO KAZI YAKE NI KUBOMOA NA SI
KUJENGA
I SHEIKH FARID NA WENZAKE WANATARAJIWA KUFIKISHWA TENAKATIKA MAHKAMA YA MWANAKWEREKWE HAPO KESHO .
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR. 24/10/2012
No comments:
Post a Comment