Na Mohammed Mhina, Zanzibar
Imeelezwa kuwa TV zote zikiwemo zile zenye migongo, matumbo na
viuno virefu zote zina uwezo sawa wa kupokea matangazo ya digitali na
Watanzania waepuke uvumi wa watu wachache wanaodai kuwa TV za zamani
hazitapokea zitafutwa mara Tanzania itakapoingia kwenye mfumo wa
Digitali.
Wito huo umetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano hapa nchini TCRA ambaye pia na Mratibu wa Ofisi za Kanda Bw.
Victor Nkya, wakati wa mkutano wa Wataalamu wa Mawasiliano ya Habadi
kwa njia ya digitali kutoka nchi za SADC unaojadili umuhimu wa mfumo wa
Digitali.
Bw. Nkya amesema kuwa wananchi hawana haja ya kuwa na hofu juu
ya TV walizonazo zikiwemo zenye matumdo na migongo mikubwa kuwa
hazitaweza kupokea matangazo ya televishen katika mfumo mpya wa
digitali.
Amesema kutokana na watu wengi kutumia televishen za Analojia,
ni lazima kila mmoja wetu awe na kingamuzi na kazi ya Mamlaka ya
mawasiliano ni kuwajengea wananchi matumaini na kuepuka kudanganywa.
Kwa siku za hivi karibuni baada ya Tanzania kuridhia mabadiliko
ya mfumo wa Digitali, wananchi wamekubwa na wasiwasi wakidhani kuwa huo
ndio mwisho wa tv za zamani.
Awali akifungua Mkutano huo wa siku tatu hapa mjini Zanzibar,
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mh. Rashid Suleiman,
amewataka wananchi kukabiliana na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza
wakati wa mabadiliko ya kutoka katika mfumo wa analojia na kuingia
katika digitali.
Amesema ni vema wananchi wakahama mapema kutoka katika mfumo huo
wa zamani ili kuepuka usumbufu wakati yatakapotokea mabadiliko hayo
kwani hakutakuwa na muda wa nyongeza kama Watanzania walivyozoea.
No comments:
Post a Comment