WAKATI
zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa wagombea wa nafasi mbali
mbali ndani ya umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM)
limehitimishwa rasmi juzi ,kashfa nzito imeibuka ndani ya UVCCM mkoa wa
Iringa baada ya wagombea wake zaidi ya robo tatu waliojitokeza wamefanya
udanganyifu mkubwa wa umri wao wa kuzaliwa.
Uchunguzi
uliofanywa na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umebaini
kuwepo kwa udanganyifu mkubwa katika ujazaji wa fomu hizo huku baadhi ya
wagombea wakiwa na umri mkubwa kuliko hata umri sahihi unaowataka
wagombea wa nafasi hiyo wawe nao wa kuanzia miaka 14-30
Sababu
ya kuwepo kwa udanganyifu huo ni baada ya kuona ushindani mkubwa katika
jumuiya nyingine za CCM katika mkoa huo huku nafasi nyeti zote katika
jumuiya hizo kama ile ya wazazi na umoja wa wanawake Tanzania (UWT)
kuchukuliwa na vigogo wa CCM .
Mmoja
kati ya vijana wanaowania nafasi moja wapo ndani ya UVCCM mkoa wa
Iringa ambaye hakupenda kutaja jina lake katika vyombo vya habari
alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa UVCCM mkoa wa Iringa imeendelea
kupoteza dira yake huku kanuni za umoja huo zikiendelea kufinyangwa na
waliopata kuwa viongozi wa umoja huo ambao bado wanaonekana
kung'ang'ania uongozi katika kundi hilo la vijana japo umri wao umepita
hata kwa mwonekano wa kawaida bila uthibitisho wa vyeti vya kuzaliwa.
Kwani
alisema inashangaza kuona vijana wengi ambao umri wao ni mkubwa
wakitumia vyeti vya kuapa mahakamani badala ya vile walivyotumia kipindi
cha nyuma ambacho walipata kuomba nafasi za uongozi ndani ya UVCCM na
jumuiya nyingine za chama.
"
Hivi tunaomba uongozi wa UVCCM mkoa kuweza kuwahoji wanachama hao
waliokimbilia kuziba nafasi za vijana wenye sifa ndani ya UVCCM kwa
kudanganya miaka yao ya kuzaliwa .....kwani haiwezekani kijana
aliyegombea nafasi ya uongozi ndani ya UVCCM mwaka 2007 akiwa na miaka
28 ama 27 leo anakuja kugombea tena katika akiwa na miaka pungufu ya
hiyo ....ina maana alisimama kukua ili kuja kugombea nafasi
hiyo.."alihoji kijana huyo
Huku
akiuhoji uongozi wa UVCCM mkoa kukubali kupokea fedha za gharama za
fomu kwa wanachama wa UVCCM ambao miaka yao imevuka mipaka ya miaka
ambayo mwanachama anapaswa kugombea katika umoja huo.
Kwani
alisema kuwa wapo baadhi ya wagombea ambao walipata kugombea nafasi za
uemnyekiti katika chaguzi za chama mwaka 2007 wakiwa wamejaza miaka 29
ila leo wamekuja na umri mdogo zaidi .
Kwa
upande wake katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa Rhoda George alisema kuwa
kila mwana chama wa UVCCM mwenye sifa ya kugombea anaruhusiwa kuchukua
fomu ila kuchukua na kurejesha sio mwisho wa mwanachama huyo kupitishwa
kuwa kiongozi kwani vipo vikao mbali mbali vya uchujaji wa majina ya
wagombea ambavyo vitapitia sifa za wote walioomba na iwapo itabainika
wamedanganya basi vikao vitaamua .
Alisema
kuwa katika kinyang'anyiro cha nafasi ya kiti ndani ya UV CCM mkoa
waliojitokeza ni wanachama 11 akiwemo Mwandishi wa habari wa gazeti la
Mwananchi Iringa , Tumain Msowoya , Mwandishi wa habari wa kituo cha
Radio Nuru Fm Aba Ngilangwa, Ramadhan Baraza ambaye ni mwalimu katika
shule ya sekondari Mwembetogwa, Charles Makoga, kanuti Mhongole, Said
Mlyuka , Fauzia Jemadari, Kaunda Mwaipyana, Asifiwe Choni na Shukru
Stivin .
Baraza
kuu la vijana Taifa wagombea waliojitokeza ni 12 na nafasi inayotakiwa
ni moja pekee ambapo wagombea hao ni pamoja na msomi wa chuo kikuu cha
Dodoma Geofrey Lukuvi , Shukru Stivin, Noel Mkanja, Asifiwe Choni,
Gaudence Kabwabwalika, Ally simba, kaunda Mhongole, Ramadhan Baraza,
Seck kasuga, Thom Masini, Kenedy Nyabusani na Thom Myinga.
Nafasi
ya moja ya mkutano mkuu wa CCM Taifa kupitia vijana imegombewa na
vijana 10 akiwemo Mary Msigala, Charles Makoga, Thom Masini, Kaunda
Mwaipyana, Noel Mkanja, Malipula Chalamila, Kinyata Likotiko, David
Edwin , Conel Malangalila na Felix Lwimbo.
katibu
huyo aliwataja wanachama waliojitokeza kuomba nafasi moja ya mkutano
mku wa CCM mkoa kupitia vijana kuwa ni hakim Mwasambogo na Baraka Mtafya
huku nafasi moja ya Halmashauri kuu ya CCM mkoa imeombwa na Nuru
Mwinuka ,Benitho Kayugwa na Baraka Mtafya.
Kwa
upande wa uwakilishi wa vijana katika mkutano wa UWT walioomba ni Nuru
Mwinuka na Janeth Inocent na uwakilishi wa UVCCM kwenda mkutano mkuu wa
wazazi waliomba ni Baraka Mtafya na Mwera Frank
Aidha
alisema Jimson Mwagama ambaye ni katibu msaidizi wa CCM mkoa wa Iringa
na Thom Myinga wao wameomba nafasi 6 kwa Tanzania bara za kuwa
kuwakilisha UVCCM katika Halmashauri kuu ya CCM Taifa wakati baraza kuu
la UVCCM Taifa lenye nafasi tano kwa Tanzania bara kwa mkoa wa Iringa
amejaza mwanachama mmoja pekee ambaye ni Asedy Mpelemwa.
WAGOMBEA WA UVCCM MKOA WA IRINGA WAINGIA MITINI KUTHIBITISHA UMRI WAO , KAMANDA WAO NA KATIBU WA CCM MKOA WATOA YA MOYONI ......
Mwanahabari na Mwanachama wa UVCCM Bi Tumain Msowoya ambaye ni mgombea nafasi ya kiti UVCCM mkoa wa Iringa Mwanachama Geofrey Lukuvi anayegombea baraza kuu la UVCCM mkoa wa Iringa
Mwanachama Fauzia Jemedari anayegombea kiti Mwanachama Gaudence Kabwabwalika anayegombea baraza kuu la UVCCM mkoa
Hawa ndio wagombea wa nafai ya UVCCM na ndio vijana wenyewe wa CCM
SAKATA la kashfa nzito kwa wana chama wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa kutuhumiwa kudanganya umri wao wa kuzaliwa limechukua sura mpya baada ya idadi kubwa ya vijana waliojaza fomu za kuomba nafasi mbali mbali katika UVCCM kukimbia kikao cha usaili kwa wagombea hao.
Huku kamanda wa umoja wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas na katibu wa CCM mkoa wa Iringa Emmanuel Mteming'ombe wakipigilia msumari kwa kutaka haki itendeke katika kuchuja majina ya wagombea wa nafasi mbali mbali bila kuwepo upendeleo wowote na wale waliochakachua miaka kuwajibishwa .
Hatua hiyo imekuja baada ya mtandao huu kuibua siri nzito ya robo tatu ya vijana hao kujaza umri wa uongo ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma miaka ya kuzaliwa ili iweze kuendena na kanuni ya UVCCM inayomtaka mgombea kuanzia miaka 14-30.
Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu juzi wakati wa kikao cha mapendekezo ya majina ya wagombea wa nafasi mbali mbali ndani ya UVCCM mkoa wa Iringa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Iringa chini ya mgeni rasmi kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas.
Sehemu kubwa ya wanachama hao walioojaza fomu hizo kushindwa kutokea katika kikao hicho nyeti cha kuhakiki taarifa walizojaza katika fomu zao za kuomba nafasi mbali mbali.
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho ambazo zimethibitishwa na baadhi ya wanachama zinadai kuwa walioshindwa kutokea katika kikao hicho ni baadhi ya wale wanaodaiwa kufanya uchakachuaji wa umri katika zoezi la ujazaji wa fomu hizo

MWANAHABARI ABBA NGILANGWA APANIA MENGI UV CCM MKOA WA IRINGA
Mwanahabari wa kituo cha Radio NuRu FM Iringa Abba Ngilangwa (pichani) ambaye ni mmoja kati ya vijana zaidi ya 10 wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa aliyejitosa kuwania nafasi hiyo amesema iwapo jina lake litapitishwa na kuwa mmoja kati ya wagombea wa nafasi hiyo ya kiti mkoa wa Iringa ana mengi ya kufanya .
Ngilangwa amesema kuwa kwa sasa ni mapema kuzungumza nini atafanya ndani ya UVCCM ila anazidi kumwomba Mungu pindi jina lake litakapopitishwa na kuwa mgombea na kushinda nafasi hiyo ataonyesha uwezo wake katika umoja huo.
No comments:
Post a Comment