Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, October 17, 2012

Vyuma chakavu vyazua kizaazaa Mikocheni jijini Dar



 Askari Polisi wakichukuwa Maelezo ya Mmoja wa Wahanga wa Mlipuko (wa pili kushoto) uliotokea mapema mchana huu maeneo ya Mikocheni kwa Warioba,Mtaa wa Nyumbu jirani kabisa na Kanisa Katoliki la Mt. Martha.

Kwa mujinu wa Mashuhuda wa tukio hilo,inasemekana kwamba kuna vijana wawili wanaofanya kazi katika nyumba moja inayokaliwa na watu wenye asili ya China,hao waliovalia fulana nyekundu,walitoka na katika nyumba hiyo na lundo la Waya zilizokuwa zimejifungafunga wakielekea kuuza kwa jamaa wa vyuma chakavu waliokuwa wakipita mtaani hapo.

Sasa wakati wanaendelea kuzikunjua waya hizo ambazo zinasadikiwa kuwa ni waya za kopa zitumikazo kama baruti za kulipuria miamba,ghafla zikafanya mlipuko mkubwa na kupelekea wasichana hao wa kazi kudhulika na mlipuko huo.ambapo mpaka sasa mmoja yuko hospitali kwa matibabu na mwingine ndie huyo anaetoa maelezo hapo.
 Wakazi wa Eneo la Jirani na nyumba hiyo wakiangalia mabashano baina ya Askari Polisi na Wachina wanaokaa kwenye nyumba hiyo ambao ni Maboss wa wafanyakazi hao walipatwa na mkasa huo.ambapo walikuwa wakiwataka waende nao kituoni kwa akiji ya kutoa maelezo.
 Mmoja wa Wahanga wa tukio hilo la Mlipuko akiingia ndani ya nyumba hiyo huku akiwa amejifunika uso baada ya kuumia na mlipuko huo.
Sehemu ya Mabaki ya waya hizo zilizolipuka na kusababisha kizaazaa mtaano hapo.

No comments:

Post a Comment