S.H.
KOVA – DCP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUMU YA POLISI DAR ES SALAAM
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA KITUO KIKUU CHA POLISI KATI
LEO
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemtia mbaroni Katibu wa Jumuiya tajwa hapo juu maarufu kama PONDA ISSA PONDA kwa makosa mbali mbali ya kuchochea vurugu na uvunjaji wa amani jijini Dar es Salaam.
Aidha
hivi karibuni Sheikh Ponda Issa Ponda aliongoza kundi la wafuasi wake
na kuvamia kiwanja No. 311/3/4 BLOCK “T” eneo la Chang’ombe katika
Manispaa ya Temeke mali ya Kampuni ya AGRITANZA ambayo ipo chini ya
Kurugenzi ya Kampuni hiyo. Mnamo tarehe 12/10/2012 Ponda Issa Ponda
aliwaongoza wafuasi wake walioteka eneo hilo wakidai kwamba wanakomboa.
Mali
za Waislamu, zilizouzwa na BAKWATA, uchunguzi wa awali umeonyesha
kwamba kiwanja hicho kina hati miliki No. 93773 uliotolewa na Wizara ya
Ardhi pamoja na mikataba mbali mbali ya kuuziana au kubadilishana kati
ya BAKWATA na Kampuni tajwa hapo juu. Pia uongozi wa BAKWATA
umeletamashahidi kuthibitisha uhalali wa kiwanja hicho kumilikiwa na
Kampuni tajwa. Hivyo watu wote waliovamia eneo hilo wakiongozwa na
Sheikh Ponda wanakabiliwa na shtaka la kuingia kwa jinai pamoja na
uharibifu wa mali katika eneo hilo. Sambamba na kukamatwa kwa Sheikh
Ponda tarehe 16/10/2012 saa 4.00 usiku karibu na eneo la maficho yake
ambapo aliletwa na pikipiki.
WATU 38 WAMEKAMATWA KWA KOSA LA KUINGIA KWA
JINAI NA UHARIBIFU
Wakati
huo huo sambamba na kukamatwa kwa Sheikh Ponda Issa Ponda Polisi
walifanya operesheni maalumu ya kuwaondoa wavamizi katika kiwanja tajwa
hapo juu kinachomilikiwa na Kampuni AGRITANZA. Watu wapatao 38 walikutwa
katika eneo la kiwanja hicho ambacho kati ya hao (7) ni wanawake na 31
ni wanaume.
Operesheni
hiyo ilifanyika tarehe 17/10/2012 usiku wa manane kuanzia saa tisa hadi
saa kumi na nusu usiku kwa muda wa dakika 90. Katika eneo hilo
vilikutwa vielelzo mbali mbali vikiwemo visu na mapanga na pia nyenzo
mbali mbali za ujenzi, pamoja na vifaa vya ujenzi, vielelezo hivyo
vimehifadhiwa katika kituo cha Polisi tayari kwa ajili ya ushahidi
mahakamani.
SHEIKH PONDA KUSABABISHA VURUGU NA VITISHO
Katika
siku za hivi karibuni Sheikh Ponda Issa Ponda amekuwa akiwaongoza
wafuasi wake chini ya Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania kwa
kufanya maandamano kinyume cha Taratibu na kuhamasisha umwagaji damu
jijini Dar es Salaam na nchini Tanzania kwa ujumla.
Kwa
ujumla Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania inayoongozwa na Sheikh
Ponda haijasajiliwa kisheria lakini wanatihumiwa kwa uchochezi wa hali
ya juu ambapo licha ya kufanya maadamano kinyume na sheria pia siku ya
tarehe 12/10/2012 walisababisha kuvunja kwa makanisa zaidi ya manane,
uharibifu wa magari na wizi au upotevu wa vifaa katika makanisa, yote
hayo yameongozwa na Sheikh Ponda na madhara yake ni makubwa.
Sheikh
Ponda amekuwa mstari wa mbele kupambana na vyombo vya dola pamoja na
kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kudai watuhumuwa waliokamatwa kwa
uvunjaji wa makanisa na kufikishwa mahakamani waachiwe mara moja kabla
siku saba na kadhalika. Uchunguzi wa watuhumiwa wote 39 unaendelea na
kufikishwa mahakamani mara baada ya kupitishwa na wakili wa Serikali
kuthibitisha mashitaka.
S.H. KOVA – DCP
KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUMU YA POLISI
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment